Accessibility links

Breaking News

Marekani yalaani mapinduzi nchini Mali


Ifuatayo ni tahariri inayoelezea sera na maoni ya serikali ya Marekani.

Rais Ibrahim Baubacar Keita wa Mali alikamatwa na jeshi Agosti 18 katika uasi wa kijeshi.

“Marekani inashutumu vikali, mapinduzi ya Mali, kama vile tunavyoshutumu aina matumizi yoyote ya nguvu katika kukamata madaraka” alisema waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo katika taarifa yake.

Wakati ikiripotiwa kwamba rais Keita ameachiliwa nyumbani kwake, inatia hofu kwamba hali ya Mali kutokuwa na uthabiti kutawaongezea nguvu wanamgambo wenye msimamo mkali katika kusongambele na agenda zao za msimamo mkali ndani ya Mali, na katika mataifa jirani, na kusababisha watu wengi kukimbia makazi yao. Hata baada ya mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2012, waasi wa kiislamu, baadhi yao ni wana uhsuiano nad Al Qaida, walishikilia uthibiti katika maeneo makubwa ya kaskazini mwa Mali, ikijumuisha mji mkuu wa kale wa kitamaduni waTimbuktu.

Katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa wa waislamu wenye msimamo mkali, raia wa Mali walilazimishwa kufuata kanuni kali za kidini, ikijumuisha ndoa za lazima kwa wanawake, mpaka pale vikosi vya Ufaransa vilipolisaidia jeshi la Mali kuwaondosha wanamgambo hao. Lakini makundi yenye silaha yameendelea kutishia raia katika maeneo ya vijijini, ghasia zimesambaa mpaka katika mataifa ya jirani ya Burkina Faso, na Niger.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, zaidi ya raia wa Afrika Magharibi 10,000 wameuwawa, na zaidi ya milioni moja wamekimbia makazi yao toka mwaka 2012.

Mwakilishi maalumu wa Marekani kwa eneo la Sahel, Peter Pham aliweka wazi katika ujumbe wake wa Twitter; Marekani haitoi mafunzo yoyote kwa vikosi vya Mali katika kipindi hiki. Pia amezungumzia katika ujumbe wa Twitter kwamba “Marekani inapinga mabadiliko zaidi ya kikatiba kwa serekali, bila kujali yanatokana na vuguvugu la mitaani ama kutoka kwa vikosi vya ulinzi na usalama.”

Marekani inaungana na jumuiya ya uchumi ya mataifa ya Afrika Magharibi, na Umoja wa Afrika, pamoja na washirika wengine wa kimataifa, katika kupinga mapinduzi ya Mali. “Uhuru na usalama wa viongozi wa serekali wanaoshikiliwa, pamoja na familia zao lazima uhakikishwe,” alisisitiza waziri Pompeo.

Marekani inatoa mwito kwa wadau wote wa kisiasa na kijeshi kufanyakazi kuirejesha serekali ya kikatiba. “Tunatoa mwito kwa washirika wote wa Mali,” alisema waziri Pompeo, “kujihusisha katika mjadala wa amani, ili kuheshimu haki za raia wa Mali katika uhuru wa kujieleza, na kukusanyika kwa amani, na kupinga ghasia.

XS
SM
MD
LG