Uharibifu umeepukwa huko Umoja wa Mataifa mwezi March pale Jamhuri ya Watu wa China, RPC, mkiukaji mkubwa wa haki miliki za kisomi, kushindwa katika juhudi yake ya kuongoza taasisi ya Umoja wa Mataifa yenye wajibu wa kulinda haki hizo, World Intellectual Property Organization.
Bahati mbaya, hali hiyo mbaya haikuepukwa mwezi October kwenye Umoja wa Mataifa. Baraza kuu la Umoja wa Mataifa lilipiga kura tena kumuweka mkiukaji mkubwa wa haki za binadamu kwenye Baraza la Haki za Binadamu, ikiwemo PRC, Russia na Cuba.
Wanaharakati wa haki za binadamu walistushwa. “Mkiukaji mzoefu wa haki za binadamu asitunukiwe kiti kwenye Baraza la Haki za Binadamu,” amesema Louis Charbonneau, Mkurugenzi wa Umoja wa Mataifa katika shirika la Human Rights Watch. Hillel Neuer, mkurguenzi mtendaji wa UN Watch ameiita hiyo ni “siku nyeusi kwa haki za binadamu.”
Katika ripoti yake ya karibuni juu ya haki za binadamu, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani iliorodhesha mlolongo wa ukiukaji mbaya wa haki za binadamu huko PRC, ikiwemo kuwatia ndani watu wengi kutoka kwa makundi ya Waislamu walio wachache huko Xinjiang.
Nchini Russia, Wizara ya Mambo ya Nje imetoa maelezo ya kina kuhusu mauaji mabaya, ukamataji holela, na ukandamizaji mbaya sana wa uhuru wa kujieleza, miongoni mwa ukiukaji mwingine.
Nchini Cuba, taifa lenye utawala wa kiimla, majeshi ya usalama ya serikali yanawanyanyasa na kuwashambulia kimwili watetezi wa haki za binadamu na wanounga mkono demokrasia karibu kila siku na kunyimwa uhuru wa kushirikiana na watu wa Cuba.
Azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa namba 60/251, ambalo liliunda Baraza la Haki za Binadamu, linawataka wanachama wake “kutekeleza kwa viwango vya juu uhamasishaji na ulinzi kwa haki za binadamu.”
Kuchaguliwa kwa PRC, Russia na Cuba mwaka huu – na Venezeula mwaka jana – kunaonyesha kuwa baraza siyo tu ni kivuli, lakini kejeli kwa kile ambacho kimepelekea kuundwa kwake.
Katika taarifa yake, Waziri wa Mambo ya Nje, Mike Pompeo alielezea kwamba Marekani ilijiondoa kutoka Baraza la Haki za Binadamu mwaka 2018, “kutokana na mwenendo wake wa kuwa dhidi ya Israel na kanuni za uanachama ambazo zinaruhusu kuchaguliwa kwa wakiukaji wabaya sana wa haki za binadamu kupewa viti katika baraza hilo.”
Alielezea kwamba kabla ya kuondoka, Marekani iliwasihi wanachama wa Umoja wa Mataifa “kuchukua hatua za haraka kufanya mageuzi katika baraza hilo kabla ya kufikia hatua ya kuwa vigumu kufanya hivyo. Bahati mbaya,” amesema, “wito huo haukushughulikiwa.”
Uchaguzi wa mwaka huu umebainisha wazi kuwa uamuzi wa Marekani kuondoka katika baraza hilo na kutumia njia nyingine na fursa za kulinda na kuhamasisha haki za binadamu ulimwenguni, amesema waziri Pompeo. “Nia yetu ya dhati inaelezwa wazi wazi katika Azimio la Ulimwengu la Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa na katika rekodi zetu za kuchukua hatua.”