Jinsi Marekani inavyowaenzi wafanyakazi kwa mchango wao

Ifuatayo ni tahariri inayoelezea sera na maoni ya serikali ya Marekani.

Jumatatu ya kwanza ya mwezi Septemba, kila mwaka, Marekani huwapa heshima wafanyakazi na kukumbuka mchango wao katika ustawi wa taifa. Mnamo Septemba 5, mwaka 1882, zaidi ya wanawake na wanaume 10,000 waliandamana katika mitaa ya Manhattan kusherehekea siku ya kwanza ya wafanyakazi.

Chama cha wafanyakazi wa New York, kiliandaa sherehe hizo ikiwa ni kuwapa heshima wafanyakazi ambao walipigania maslahi bora, na kupunguziwa saa za kufanya kazi, lakini pia hali nzuri makazini kwa wafanyakazi wote. Pia ilikuwa ni siku ambayo wafanyakazi hao walisamehe mshahara wao wa siku hiyo kuandamana katika kupigania kuongezeka kwa maslahi kwa kazi zao ngumu.

Kwa mwaka huu, janga la Covid-19, limeleta changamoto mpya kwa wafanyakazi, matatizo ambayo hayajawahi kutokea kabla. Wakati mamilioni ya wafanyakazi kwa miezi kadhaa wanafanyia kazi majumbani kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona, maelfu ya watu waliitwa ili kupambana na ugonjwa huu. Wafanyakazi wa dharura na afya walijitolea maisha yao kuwa mstari wa mbele kusaidia waliougua, na kuwaliwaza waliofariki dunia, na ukweli ni kwamba mamia ya wafanyakazi wa afya wamejikuta wakihatarisha maisha yao na kuambukizwa.

Na pia kuna mamilioni ya wengine, wengi wao wakifanyakazi katika ajira za kipato cha chini, ambao wamejitolea kufanya taifa lisonge mbele. Vyakula lazima vizalishwe, kuandaliwa, kufikishwa sehemu stahiki na kuuzwa ili wengine waweze kula. Barua lazima zisafirishwe, kugawanywa na kusambazwa kote nchini. Wote ambao wanahakikisha huduma za umeme na maji zinaendelea vilevile wana umuhimu katika kuhakikisha wengine wanaishi kuliko viongozi wa kisiasa kote nchini ambao wamekuwa wakiandaa mwitikio wa kusambaa kwa virusi vya corona ama kutafuta njia mpya ya kupatikana vifaa vya kujikinga na vya afya.

“Katika kutoa heshima, dunia kwa mara nyingine imeshuhudia nguvu isiyoshindikana ya Marekani.” Amesema rais Donald Trump.

“Kote nchini mwetu, mashujaa wametekeleza. Madaktari, na wauguzi wanafanyakazi usiku na mchana kuokoa maisha. Wakulima, madereva wa malori, na wazalishaji chakula wanafanyakazi kuhakikisha ghala zetu za vyakula zimejaa na watu kupata chakula. Familia zinawasaidia majirani wenye mahitaji, na jamii zao zinategemea umoja wao kukabiliana na janga hili,” amesema.

“Lakini ni heshima kwa taifa hili, na watu wa nchi yetu wamefanikiwa kufanya lililowezekana, na maisha yameokolewa.