Kuendelea Kuhimiza Dini Kuvumiliana Nchini Indonesia

Ifuatayo ni tahariri inayoelezea sera na msimamo wa serikali ya Marekani.

Marekani ilikuwa nchi ya kwanza kuanzishwa kwa kuzingatia haki za msingi za kila mtu.

“Haki ya msingi zaidi kati ya zote ni uhuru wa kujifanyia maamuzi na kuabudu” amesema waziri wa mambo ya nje wa Mike Pompeo.

Pompeo amesema kwamba dhamira kubwa ya kitaifa ni kuheshimu haki za msingi ambazo zimeletwa na mwenyezi mungu.

Hii ndio sababu Marekani ilikuwa na msimamo dhabithi kati ya nchi za magharibi katika kuunga mkono Indonesia kupata uhuru wake kutoka kwa utawala wa ukoloni na imekuwa mtetezi mkubwa wa kuunga mkono juhudi za demokrasia nchini Indonesia kwa miongo miwili iliyopita.

Kwa watu wetu kuzingatia uhuru na kustahimiliana ni jambo muhimu sana.

Lengo kubwa la kuwepo demokrasia nchini Indonesia ni kutaka kuona kwamba watu wote kutoka dini mbalimbali wanaishi kwa kuelewana.

Hili lipo katika katiba ambayo inasema kwamba kila mtu ana uhuru wa kuabudu.

“Hakuna kabisa sababu kwamba waislamu hawawezi kukaa Pamoja na wakristo au dini nyingine.” Amesema waziri Pompeo.

“Utamaduni wa watu wa Indonesia wa kuvumiliana na kuishi kwa Pamoja ni lazima uendelee kudumu daima,” amesema Pompeo.

“Shutuma za kuchafuana kidini ambazo husababisha vifo zimekuwa za kawaida. Utengano wa kidini umewadunisha baadhi ya watu wa dini mbalimbali na kudhulumiwa na kujiona watu wa hadhi ya chini sana.”

Waziri Pompeo ameendelea kusema kwamba viongozi kadhaa wa dini zote wanastahili kuzungumzia swala hili kwa niaba ya watu wote kutoka dini mbalimbali, haki zao zinapokiukwa. Ameendelea kusema kwamba kuna haja ya viongozi wengi wa dini kuwa mashahidi wa maadili mema.

Mojawapo ya sehemu hizo ni Burma ambapo jeshi limewadhulu watu wa Rohingya na wengine kutoka jamii ndogo ndogo.

Indonesia imesurutisha mataifa ya ASEAN kuajibika kuhusu haki za kibinadamu, lakini haki haijapatikana. Amesema waziri Pompeo.

Lakini tisho kubwa kwa hali ya baadaye ya uhuru wa kuabudu, kulingana na Pompeo ni chama cha kikomunisti kinachotawala China, ambacho kinaendeleza vita dhidi ya watu wa dini mbalimbali kama waislamu, wakristo, wabudha na wengine.

“Haki za msingi alizotoa mwenyezi mungu ni kwa kila mtu,”

Amesema waziri Pompeo. “Hiyo ndio sababu watu walio huru katika mataifa hutu wanastahili kulinda haki zao.”