Marekani haijawahi kuidhinisha mkataba wa Rome uliounda mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC kwa sababu ya maswala kama uhuru wa nchi.
Mahakama ya ICC imeacha kazi yake ya kuchunguza uhalifu dhidi ubinadamu na mauaji ya kimbari, malengo ya Marekani, na imeanzisha uchunguzi wenye ushawishi wa kisiasa dhidi ya wanajeshi wa Marekani.
Imepuuza kutilia maanani mifumo ya kisheria na ya kijeshi ya Marekani ambao unaowawajibisha maafisa wa Marekani.
Balozi wa Marekani anayehusika na haki ya jinai ulimwenguni Morse Tan, amesema kwamba mahakama ya ICC haijafanya kazi yake inavyostahili. Inastahili kuwa mahakama ya mwisho kabisa. Na kwamba Marekani tayari imeshugulikia uchunguzi kuhusu maafisa wake wa kijeshi.
Ili kuwakinga wanajeshi wa Marekani dhidi ya kufunguliwa mashtaka kwa njia isiyokuwa ya kisheria, Marekani imewawekea vikwazo vya kiuchumi mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Fatou Bensouda na mwanachama mkuu wa timu ya uongozi wa mahakama hiyo Phakiso Mochochoko.
Balozi Morse Tan amesema kwamba “mahakama ya ICC imeingizwa katika siasa, ufisadi. Tuna Ushahidi. Na haya siyo mambo ambayo mahakama inatakiwa kuyafanya. Imehukumu kesi 4 za uhalifu kutokana na mkataba wa Rome na hukumu moja ipo katika mahakama ya rufaa.
Marekani imefanya mambo mengi zaidi kuliko mahakama ya ICC ilivyofanyakatiak misingi hiyo hiyo. Tuna maadili sawa, lakini kwa hakika tunafanya kwa njia ambayo ni zaidi kuliko yale ambayo ICC imefanikiwa kufanya.