Marekani Yasimamia Mkataba Wa Amani Kati Ya Sudan Na Israeli

Marekani imesimamia makubaliano ya amani kati ya Sudan na Israeli, ikiwa ni makubaliano ya tatu kati ya Israeli na taifa hilo lenye waislamu wengi chini ya miezi mitatu.

Israeli na Sudan zimekubaliana kurekebisha uhusiano wao. Nchi hizo mbili zitaanza mashauriano juu ya makubaliano ya ushirikiano katika kilimo, uchumi, biashara, usafiri wa anga, maswala ya uhamiaji, na maeneo mengine ya faida kwa pande zote.

Mkataba huu wa amani wa kihistoria unafuata makubaliano kama hayo kati ya Israeli na Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain. Upanuzi wa Makubaliano ya Abraham kuijumuisha Sudan ni hatua muhimu ambayo itatoa fursa kwa Sudan na Israeli kuboresha maisha ya watu wao wakati ikiimarisha usalama wa nchi zote mbili.

Kwa kweli, kwa miongo kadhaa, Sudan ilikuwa katika hali ya vita na Israeli na ilisusia bidhaa za Israeli. Baada ya Vita vya Siku Sita mnamo 1967, Jumuiya ya Mataifa ya Kiarabu ilikutana Khartoum ambako walitoa kile kilichojulikana kama azimio la Hapana la nyanja tatu: hakuna amani, hakuna kutambuliwa, na hakuna mazungumzo.

Hayo yote yamebadilika kama Mshauri Mwandamizi wa Rais, Jared Kushner alivyosema: "Tuna Nyanja tatu chini ya Rais Trump: Tuna amani, tunatambuliwa, na tuna mazungumzo kwa amani zaidi.

Baada ya kuishi kwa miaka mingi chini ya udikteta mkali wa Kiislamu uliounga mkono ugaidi, watu wa Sudan wana serikali mpya na sera mpya, alisema Rais Trump: "Serikali ya mpito ya Sudan imeonyesha kujitolea kwake kupambana na ugaidi, kufungua fursa ya soko la uchumi, na kukuza taasisi ya kidemokrasia ambayo inakuwa. Mkataba wa leo unajengwa juu ya ahadi hizo na unaashiria mabadiliko muhimu katika historia ya Sudan."

Marekani inakaribisha maendeleo haya muhimu na iko tayari kusaidia watu wa Sudan wanapofanya kazi ya kujijengea maisha bora ya baadaye na vizazi vijavyo.

Shukrani kwa makubaliano mapya matatu ya amani, Mashariki ya Kati na Afrika wanapata mabadiliko makubwa ya kijiografia. Kadiri nchi zaidi zinarejesha mahusiano na Israeli, eneo hilo litakuwa thabiti zaidi, salama, na kufanikiwa.

Marekani itaendelea kusimama na watu wa eneo hili wakati wanafanya kazi ya kujenga siku zijazo zenye mwanga na matumaini zaidi.