Machafuko ya kisiasa nchini Belarus tangu kuchaguliwa tena kwa njia ya udanganyifu kwa kiongozi wa kiimla Alexander Lukashenko hapo Agosti 9 yanaendelea.
Wanachama wa upinzani wa kisiasa nchini Belarusi waliunda Baraza la Taifa la Uratibu, au NCC, kushauriana na mamlaka ya Belarusi juu ya kuitisha uchaguzi huru na wa haki na makabidhiano ya madaraka.
Badala ya kujihusisha kwa nia njema, utawala wa Lukashenka umeanzisha uchunguzi wenye ushawishi wa kisiasa dhidi ya Baraza hilo la taifa la Uratibu na kuwatia ndani, kulazimishwa kwenda uhamishoni, na kuwateka nyara wanachama wa NCC.
Kwa kweli, Marekani ina wasiwasi mkubwa na utekaji nyara wa Septemba 7 wa mwanachama wa Baraza la taifa la Uratibu Mariya Kalesnikava mjini Minsk, na kufukuzwa kwa nguvu kwa Msemaji Anton Rodnenkou na Katibu Mtendaji Ivan Krautsou hapo Septemba 8. Maxim Znak, pia mwanachama wa Baraza la taifa la Uratibu, alikamatwa siku iliyofuata.
Marekani inapongeza ujasiri wa Bi. Kalesnikava na watu wa Belarusi kwa kusisitiza kwa amani haki yao ya kuchagua viongozi wao katika uchaguzi ulio huru na wa haki.
Waandamanaji wamekabiliwa na ghasia kali na ukandamizaji na mamlaka ya serikali, ambayo ni pamoja na kupigwa mchana kweupe na maelfu ya watu kuwekwa mahabusu, pamoja na ripoti zinazoongezeka za utekaji nyara.
Tangu Septemba mosi, wanafunzi wa vyuo vikuu wamekuwa waathirika wa ukandamizaji mkali ulioongozwa na vikosi vya usalama vilivyovaa nguo nyeusi na kufunika nyuso zao na kofia nyeusi za mchezo wa kwenye barafu. Watu kadhaa walichukuliwa kutoka mitaani na kutupwa kwenye mabasi madogo yasio na namba.
Marekani ikishirikiana na washirika wake inazingatia kuweka vikwazo zaidi vinavyolenga kuhamasisha uwajibikaji kwa wale waliohusika katika ukiukwaji wa haki za binadamu na ukandamizaji huko Belarusi. Tunaikumbusha mamlaka ya Belarusi juu ya jukumu lao kuhakikisha usalama wa Bi. Kales-nikava na wale wote wanaoshikiliwa kinyume cha sheria alisema waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo katika taarifa yake.
Tunatoa wito kwa mamlaka ya Belarusi kumaliza vurugu dhidi ya watu wake, kuwaachilia huru wale wote ambao wamewekwa kizuizini kinyume cha sheria ikiwa ni pamoja na raia wa Marekani Vitali Shkl-iarov, na kushiriki katika mazungumzo ya maana na wawakilishi wa kweli wa jamii ya Belarusi.