Accessibility links

Breaking News

Bahrain yarejesha mahusiano ya kidiplomasia na Israeli


Ifuatayo ni tahariri inayoelezea sera na maoni ya serikali ya Marekani.

‘Katika kipindi cha chini ya mwezi mmoja, Marekani imesimamia mikataba ya kihistoria ya amani huko Mashariki ya Kati, wa karibuni ukiwa kati ya Israel na Bahrain. Wa kwanza ukiwa kati ya Israel na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Katika azma ya kuleta amani na ushirikiano, Bahrain imekubali kurejea uhusiano wa kawaida wa kidiplomasia na Israel. Watafungua ofisi za ubalozi na mabalozi, wakianza na safari za ndege za moja kwa moja kati ya nchi zao, na kuanzisha ushirikiano katika sekta mbali mbali, ikiwemo afya, biashara, teknolohia, elimu, ulinzi na kilimo.

Ilikuwepo mikataba miwili tu mingine ya amani na Israel katika muda wa miaka 72 iliyopita, amesema Rais Trump, “nina matumaini makubwa sana kwamba kutakuwa na mingine itakayofuata.” Kwa hakika, mikataba na Bahrain na Umoja wa Falme za Kiarabu pia itasaidia kusukuma mbele matarajio ya kupatikana kwa haki na amani ya kudumu kati ya Israel na wapalestina.

Baada ya miongo kadhaa ya ukosefu wa uthabiti na mizozo, hali katika Mashariki ya Kati imeboresha kwa kiasi kikubwa sana katika muda wa miaka mitatu iliyopita, amesema Rais Trump.

“Nimerejesha uaminifu na washirika wetu katika eneo hilo, na kwa pamoja tumetokomeza ukhalifu wa ISIS kwa asilimia 100; tumwatenga wale wenye msimamo mkali ambao watumia uislamu kupanda mbegu za ukosefu wa uthabiti. Hivi leo, mataifa kote katika eneo hilo na kwingineko duniani wanaungana pamoja, wanaungana kwa azma ya kujenga hali njema ya baadaye, mbali na uadui ambao unachochea vitisho.”

Rais Trump amewashukuru viongozi wa Israel na Bahrain kwa ushujaa wao kusukuma mbele mkataba wa kihistoria.

“Uongozi wao unathibitisha kwamba hali ya baadaye inaweza kujaa matumain na haihitaji kutawaliwa na mizozo ya siku za nyuma. Nchi nyingi zitakaporejesha uhusiano wa kawaida na Israel – hili litatokea haraka sana, tunaamini – eneo hilo litakuwa na uthabiti mkubwa sana, na mafanikio.”

Marekani itaendelea kusimama na watu wa Mashariki ya Kati wakati wakifanya kazi ya kujenga hali njema na yenye matumaini zaidi kwa siku za usoni.

XS
SM
MD
LG