Accessibility links

Breaking News

China Inaendelea Na Mchezo Hatarishi


Ifuatayo ni tahariri inayo eleza mtazamao na maoni ya serikali ya Marekani.

Jamhuri ya watu ya China (PRC) inajihusisha kwenye mchezo hatari wakati ikikusudia kuongeza maradufu viwango vya silaha zake za nyuklia katika muda wa muongo mmoja. Kwenye taarifa za hivi karibuni kutoka kwa waziri wa zamani awa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alisema kuwa, “Beijing imekata kufichua idadi yake ya silaha, na ni ngapi inapanga kuongeza au kuzitumia.” China ndilo taifa linalotoa ushirikiano mdogo zaidi miongoni mwa wanachama watano wa kudumu kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Licha ya usiri wa chama cha kikomunisti cha China, ulimwengu haujui kwamba Beijing inaendelea kufanya majaribio yake ya nyuklia ardhini, angani na kwenye bahari na kwamba pia imeendelea kupanua na kuimarisha program zake wakati ikikataa kutoa ushirikiano kwa Marekani kuhusiana na hali hiyo.

Picha za satellite zimeonyesha jeshi la China la People’s Liberation, PLA, likijitahidi kuunda jeshi la kimataifa kufikia 2049. Mkutano wa hivi karibuni ulioitishwa na PLA ulionyesha silaha mpya aina ya Dongfeng-41 zenye uwezo wa kufikia Marekani ndani ya dakika 30.

Pompeo alisema kuwa PLA imepanga kutumia silaha hizo katika siku za karibuni na kuwa iwapo hali hiyo itanedelea China itaongeza maradufu uwezo wake wa silaha za nyuklia katika kipindi cha muongo mmoja ujao.

Kando na kuimarisha uwezo wake wa nyuklia, PLA imeweka zaidi ya silaha 1,000 za makombora karibu na ufukwe wake. Nyingi ya silaha hizo huenda zikawa zenye nyuklia au aina nyingine ya vilipuzi. Pompeo ameonya kuwa silaha hizo zinalenga vikosi vya Marekani mashariki mwa Asia pamoja na kuzua hofu miongoni mwa washirika wake huku PLA ikisukuma ajenda yake ya kigeni.

Program ya nyuklia ya Beijing imeendelea kuimarika wakati ikiwa tishio kwa majirani zake wasio na uwezo huo na kwa hivyo kutilia mashaka mkataba usioeleweka vyema wa NO FIRST USE unaohitaji kila taifa lenye nyuklia kuwa na uwazi. Marekani pamoja na mataifa mengine huwa wana uwazi pamoia heshima kwa sheria za kimataifa za nyuklia zilizowekwa huku wakikweka mikakati ya kuzuia mashidano mashindano ya kinyuklia.

“Tunashiriki kwenye mawasiliano ya kutegemewa na mataifa mengine yenye uwezo wa nyuklia na tunasihi Beijing kutoa ushirikiano.” Amesema Pompeo.

Waziri wa zamani Pompeo amewaomba viongozi wa PRC kushirikiana na Marekani na Russia katika kutengeneza mikakati mipya ya udhibiti wa silaha za nyuklia.

Pompeo amewasihi marafiki wa Marekani kuzungumza. “ Mataifa yanayounga mkono udhibiti wa silaha na yanayotegemea uwezo wa Marekani wa kuzuia, yameendelea kukaa kimya kuhusiana na uimarishaji wa silaha wa nyuklia.

Historia imeweka dhahiri kuwa mataifa yenye nguvu ikiwemo China yana jukumu la kuwajibika kuhusiana na selaha hatari zaidi ulimwenguni. Mataifa yanayounga mkono mataifa yasiowajibishwa au kukashifu matendo yao mwishowe ndiyo huumia.


XS
SM
MD
LG