Accessibility links

Breaking News

Cuba yamwachia huru mwanahabari aliyekuwa mfungwa wa maoni


Ifuatayo ni tahariri inayoelezea sera na msimamo wa serikali ya Marekani

Mwanahabari wa kujitegemea wa Cuba, Roberto de Jesus Quinones hatimaye ameungana tena na familia yake, baada ya mwaka moja wa mateso kama mfungwa wa maoni nchini Cuba.

Huku akifurahiswa na kuachiliwa kwake, Marekani inalaani vikali kwa mara nyingine kufungwa kwake kinyume cha sheria, kwa kosa pekee la kufanya kazi yake, waziri wa mambo ya nje wa marekani Mike Pompeo alisema katika taarifa.

Tarehe 7 Agosti mwaka 2019, serikali ya Cuba ilimkuta na hatia Quinones kwa mashtaka yasioeleweka ya kupinga na utovu wa nidhamu, na kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja katika kambi ya mafunzo. Kuzuiliwa kwake na kesi yake viligubikwa na kupuuza kabisa kanuni za kisheria.

Viongozi wa Cuba hawakumjulisha Quinones mashtaka dhidi yake hadi dakika chache kabla ya kesi kuanza na hawakumruhusu uwakilishi wa kisheria mahakamani.

Waendesha mashtaka walimzuia Quinones kuwasilisha ushahidi wa majeraha aliyopata alipokuwa mikononi mwa polisi waliomkamata. Mwezi machi, alinyimwa msamaha.

“Ni jambo la aibu kuona serikali ya Cuba ilimfunga mwanahabari ambaye uhalifu wake pekee ni kuifanyia kazi jamii inayotaka uwazi zaidi”, amesema waziri Pompeo.

“Pia haishangazi. Utawala hutumia kisingizio chochote kuwanyamanzisha wakosoaji wake na kukiuka haki za binadamu, ikiwemo haki za uhuru wa kujieleza na dhamana ya kesi kuendeshwa kwa haki.”

Cuba bado ni taifa la kanda ya Amerika ambalo linakandamiza vyombo vya habari, kwa mujibu wa kamati ya kuwalinda waandishi wa habari, CPJ.

Taasisi hiyo pia imeiorodhesha Cuba miongoni mwa mataifa 10 ya juu duniani yanayokagua zaidi vyombo vya habari.

Magazeti na vyombo vya habari vya utangazaji vyote vinadhibitiwa na serikali ya kikomunist ya Cuba, na kisheria, vyombo hivyo vyatakiwa kufanya kazi kulingana na malengo ya jamii ya ujamaa.

Marekani inatoa wito kwa washirika wake wa kidemokrasia kote ulimwenguni, kuheshimu haki za binadamu pamoja na uhuru wa vyombo vya habari, ikiwa ndilo sharti la ushirikiano wowote na Cuba.

XS
SM
MD
LG