Uhuru wa kuabudu ni haki ya msingi ambayo ina-ainishwa katika ibara ya kwanza ya katiba ya Marekani. “Bunge halitatunga sheria isiyoheshimu kuanzishwa kwa dini, ama kukataza uhuru wa kuabudu.”
Peter Berkowitz, mkurugenzi wa mipango ya sera wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, amesema kuna uhusiano baina ya mataifa ambayo yanalinda uhuru wa kuabudu, na yale yanayoheshimu haki za msingi.
“Tunafahamu likiwa ni jambo muhimu, uhusiano wa juu baina ya nchi zinazolinda uhuru wa dini, na mataifa ambayo yanalinda uhuru mwingine wowote ambao Marekani kidesturi imekuwa ikiujali. Na njia hii inaleta maana kama utalinda uhuru wa kuwa na maoni tofauti kuhusu moja ya masuala ambayo binadamu amekabiliana nayo kwa kipindi kirefu. Mtazamo tofauti kuhusu mungu.”
Kuna nchi zenye utawala wa kiimla, ikijumuisha China, Iran, na Russia ambazo zinatamka kwa sababu Marekani haifanyi kwa usahihi kushikilia haki za binadamu nyumbani kwake, haina haki ya kuhamasisha haki hizo kwenye mataifa ya nje.”
Lakini mkurugenzi Berkowitz anazungumzia mtazamo huu unastaajabisha.
Kuna tofauti ya msingi kati ya nchi za kiliberali kama vile Marekani, ambayo yamejengwa kwa kuzingatia haki za binadamu, na nchi kama China, Iran, Russia ambazo zinapinga wazo la haki za binadamu. Kwa hakika, sina maana kwamba kukataa hilo kama kuna wale wenye ushujaa wa kupinga haya ndani ya Russia, China na Iran. Tunajua kwamba wapo. Lakini hali ya kisiasa katika jamii kiujumla hairuhusu kuwa na mazungumzo kama hayo.”
Tangazao la uhuru la Marekani na azimio la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, amesema mkurugenzi Berkowitz, linaangukia katika kifungu cha nne ya hali ya kimataifa ya kutathimini aina zote za serikali, na namna serikali hizo zinapaswa kuwajibika. Pia ameelezea matumaini yake kwa watu wanaojitokeza kutetea hilo. Demokrasia ya kileberali, ni aina ya serikali inayojali haki za binadamu.”