Accessibility links

Breaking News

Fikra Za Ubunifu Zinahitajika Kuwasaidia Wananchi Wa Venezuela


Ifuatayo ni tahariri inayoelezea mtazamo na maoni ya serikali ya Marekani.

Utawala mbaya na rushwa katika serikali haramu ya Nicolas Maduro imeitumbukiza Venezuela kwenye hali mbaya sana ya kibinadamu, kisiasa na kiuchumi katika historia ya nchi.

Marekani imekuwa ikitoa misaada ya mamilioni ya dola katika juhudi za misaada ya kwa ajili ya watu Venezuela wote walioko nje na ndani ya nchi. Hata hivyo utoaji wa misaada ya kibinadamu ni suluhisho la muda mfupi. Kunahitajika mawazo mapya kwa masuluhisho ya muda mrefu.

Ni kutokana na sababu hiyo ndipo shirika la kimataifa la marekani la kutoa misaada USAID kwa ushirikiano na benki ya maendeleo ya Marekani wamezindua mpabgo unaojulikana kama Better Together.

Aliyekuwa mkurugenzi wa maabara ya Global Development katika USAID Harry Bader anasema kuwa Better Together ni APP inayokaribisha ubunifu kutoka kila upande wakati wowote na kote ulimwenguni, katika kutoa maoni yanayoweza kuchangia utoaji wa misaada kwa watu wa Venezuela walioko nje na ndani ya nchi. Maabara hiyo imeanza kugeuka kuwa taasisi ya ubunifu, teknolojia na utafiti ikiwa sehemu ya taasisi ya Demokrasia, Maendeleo na Ubunifu.

Watu ambao wamepitia matatizo na ugumu wa maisha na kunyimwa kimaisha nchini Venezuela na hivyo kukimbia utawala na kujaribu kubuni njia za kujijenga kwa muda kimaisha nje ya nchi, wanaweza kutumia ujuzi wa binafsi na kuendeleza mawazo ambayo hakuna idara ya maendeleo ingeweza kufahamu au kuwa na uwezo wa kufikiria hayo, kwasababu si juu yetu kufanya hivyo. Ni maisha ambayo ya wavenezuela ndio yanaweza kugeuzwa kuwa ni wazo abao watatafuta ubunifu.

Ni jambo la kutia hamasa kuhusu tuzo hizi ama zinaweza kuwa kubwa au ndogo, amesema bwana Bader.

“Tunafanya hii miradi kama vile ya fursa ya upatikanaji maji safi. Tunabuni mabaraza ya kidigitali kuwasaidia watu kutafuta jamaa zao. Tunaunda mabaraza kuwasaidia watu kutafuta ajira kwa mujibu wa kanuni na taratibu za nchi husika ambapo wanajikuta wapo, ambao wanaweza kuhamia kutafuta usalama na kuzisaidia familia zao.”

Kama sehemu ya mradi wa Better Together, USAID inashirikiana na watu wa Venezuela ndani na nje ya nchi pamoja na watu wa Brazil, Peru, Colombia yakiwemo makundi mengine ya kutoa misaada kote katika ukanda wenye huo.

Mwishoni mwa mwezi Oktoba, kaimu naibu mratibu wa USAID John Barsa alitangaza kundi la karibuni kabisa kupokea misaada ya USAID.“Nimeridhishwa sana kutangaza hivi leo kuwa USAID inafadhili miradii mitatu mipya nchini Venezuela, Chile na Colombia yeye thamani ya dola milioni 1 chini ya mradi wa Better Together.”

Ameongeza kusema kuwa misaada hiyo itaboresha maisha ya maelfu ya watu wakati miradi inayofadhiliwa na USAID na benki ya IDB ikifikia 19 kwenye mataifa hayo huku mingine kadhaa ikisubiriwa.

Kwa taarifa zaidi kuhusu mradi wa Better Together Challenge, unaweza kutembelea www.JuntosEsMejorVE.org.

XS
SM
MD
LG