Accessibility links

Breaking News

Haki za msingi na kwa nini ni muhimu


Ifuatayo ni tahariri inayoelezea sera na maoni ya serikali ya Marekani.

Katika tangazo la Uhuru, waanzilishi wa taifa la Marekani walifafanua haki zinazoweza kupatikana kama vile maisha, uhuru, na kutafuta furaha. Haki hizi zinachukuliwa ni za asili kwa watu wote na takriban kile tunachoaminisha leo tunaposema haki za binadamu, alisema Peter Berkowitz, mkurugenzi wa mipango ya sera wa wizara ya mambo ya nje .

Haki hizi haziwalindi Watu Wamarekani tu nyumbani bali zinaunda msingi wa maadili wa sera ya mambo ya nje , alisema Bwana Berkowitz.

Anaendelea kusema : “Tulichukua majukumu ya kutetea mnamo mwaka 1948 wakati tuliongoza juhudi katika Umoja wa Mataifa kupitisha Azimio la Ulimwengu la Haki za Binadamu. Kumekuwa na marais kutoka vyama vyote vya siasa ambao wamepigania haki za binadamu. Na ahadi za kuanzishwa taifa la Amerika zilihusisha kuheshimu utu ambao unawahusu wanadamu wote.”

Mwaka mmoja uliopita, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo aliitisha Tume ya Haki zisizoweza kushikamana na upande wowote ikiwa na mamlaka maalum, alisema Mkurugenzi Berkowitz.

“Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo aliwataka wanachama wa tume kuchunguza, kubainisha bila ya shaka yeyote nia ya dhati ya Marekani kwa haki za binadamu katika sera ya mambo ya nje, kama ilivyoelezewa katika nyaraka za azimio la uhuru, na katiba ya Marekani -- na pia kusaidia kuelewa bila shaka yoyote nia ya dhati ya Marekani kwa haki za binadamu hasa ukizingatia azimio la ulimwengu la Haki za Binadamu, ambalo tumetia saini mwaka 1948,” alieleza zaidi.

Haki zisizoegemea upande wowote huathiri moja kwa moja uhusiano wa Marekani na nchi binafsi, alisema Mkurugenzi Berkowitz.

“Tunaona, kwa mfano, waziri Pompeo mara kwa mara akilaani juu ya kufungwa kwa waislam Waighur katika kambi za mafunzo za Wachina. Tuliona katika miaka ya 1980 wakati Ronald Reagan alipotetea haki za kibinadamu za wapinzani kwamba Umoja wa Sovyeti ulikuwa umewafunga kikatili. Tunasikia wakati utawala unaishambulia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambayo pia inawanyanyasa raia wake,” alisema Berkowitz.

Ingawa haki za kibinadamu sio jumla ya sera zote za kigeni za Marekani, alibainisha Mkurugenzi Berkowitz, hiyo ni sehemu moja muhimu ya mchanganyiko wa sera za mambo ya nje za Amerika.

XS
SM
MD
LG