Accessibility links

Breaking News

Hatua ya Kupambana Na Ufisadi Lebanon


 Ifuatayo ni tahariri inayoelezea sera na msimamo wa serikali ya Marekani.

Kwa zaidi ya mwaka mmoja, watu wa Lebanon wamekuwa wakiandamana barabarani wakitaka mabadiliko ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.

Wamechoka kuishi katika nchi ambayo hali ni mbaya, ikiwemo kupanda kwa mfumuko wa bei, ukichanganya na miundo mbinu mibovu, maji chafu na umeme usiokuwa na uhakika -- wakati viongozi wa kisiasa wanaendelea kujilimbikizia mali na kukataa kutekeleza mageuzi yanayohitajika.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo alizungumzia hali ya Lebanon katika kikao na waandishi wa habari hivi karibuni.

“Watu wa Lebanon wanataka viongozi wa kisiasa ambao wamejaa ufisadi kama wa Hezbollah, kuacha kuiharibu nchi yao.” Amesema Pompeo

Novemba 6, Marekani ilichukua hatua ya kuwasaidia watu wa Lebanon katika juhudi zao za kutaka mageuzi na uwajibikaji.

Ofisi ya kudhibiti mali za nje katika Wizara ya Fedha ya Marekani, ilimuwekea vikwazo Gibran Bassil rais wa chama cha siasa cha Free Patriotic Movement na aliyekuwa waziri katika baraza la mawaziri la Lebanon.

Chama cha Free Patriotic Movement ni mshirika muhimu wa Hezbollah.

Bassil aliwekewa vikwazo kulingana na amri ya kiutendaji namba 13818 inayosimamia uwajibikaji wa sheria ya kimataifa ya haki za kibinadamu, inayolenga visa vya ufisadi na ukiukwaji wa haki za binadamu kote duniani.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema kwamba vikwazo vya Marekani dhidi ya Bassil vinafuatia na kuzingatia “hatua ya hivi karibuni ya kutaja baadhi ya maafisa wa Lebanon chini ya amri ya kiutendaji ya kupambana na ugaidi namba 13224, ambao ni Yusuf Finyanus na Ali Hassan Khalil, binafsi wanajali maslahi yao na ya Wahezbollah wanaoungwa mkono na Iran, badala ya maslahi ya watu wa Lebanon.”

Kwa kupitia vitendo vya ufisadi, Bassil pia alidhoofisha mfumo wa utawala bora na kuchangia katika kuenea ufisadi na utawala mbovu wa kisiasa unaoikumba Lebanon, ambao umetoa kinga kwa kundi la Hezbollah na vitendo vyake vya kutatiza utawala.”

Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo amesema kwamba muda umekwisha kwa wanasiasa wa Lebanon “kuacha maslahi binafsi na kuwafanyia kazi watu wa Lebanon.”

“wanataka nchi iliyo huru. Wanataka nchi inayojitawala. Hawataki viongozi wa kisiasa ambao ni mafisadi na wanaonufaika na mfumo wa ufisadi ambao wamejiwekea ili kuibia nchi yao. Wanataka kuwa huru, wanataka maendeleo, wanataka kazi.”

Hayo ndio mambo ambayo Marekani inataka yafanyike Lebanon, amesema Waziri wa Mambo ya Nje Pompeo: “na vikwazo tunavyoweka dhidi ya aliyekuwa waziri, ni muhimu katika kutupeleka katika hatua ambayo siku moja, watu wa Lebanon wanaweza kupata kile ambacho wanastahili kupata.”

XS
SM
MD
LG