Accessibility links

Breaking News

Hatua Za Kuzuia Utawala Wa Cuba Kuwakandamiza Wananchi Wake


Ifuatayo ni tahariri inayoelezea sera na maoni ya serikali ya Marekani.

Marekani inachukua hatua kuuzuia utawala wa Cuba kuwanyonya watu wake kiuchumi na kutumia pesa hizo kufadhili serikali haramu ya Venezuela inayoongozwa na Nicolas Maduro.

Serikali ya Cuba inatumia mbinu mbaya sana kupata fedha. Inaiba pesa zinazotumwa na watu wanaoishi nje ya Cuba kwa familia zao na marafiki walio ndani ya nchi hiyo.

“Cuba ni nchi pekee ulimwenguni ambako wanajeshi huchukua makato katika pesa zinazotumwa kutoka nje,” amesema kaimu waziri mdogo wa maswala ya ukanda wa magharibi balozi Michael Kozak wakati wa maalum cha karibuni kilichofanyika kuzungumzia wasi wasi wa haki za binadamu nchini Cuba.

“Jeshi la Cuba lilikamata pesa kwa malengo yake, na kuzitumia kufadhili uingiliaji nchini Venezuela na kuimarisha biashara zake ambazo hazipati faidha. Wanachukua sehemu ya makato hayo na kuwalazimisha watu wa Cuba kutumia pesa zao zilizobaki katika zile walizotumiwa, kununua bidhaa kwa bei kubwa katika maduka yanayodhibitiwa na serikali.”

Ili kumaliza utaratibu huu, Marekani imeweka vizuizi dhidi ya jeshi la Cuba kuchukua pesa za raia wa Cuba wanazotumiwa na watu wao walio nje ya nchi. Wakati huo huo, Marekani imeruhusu fedha hizo ziweze kutumwa kutumia mashirika binafsi na ya kiraia.

Marekani pia inataka jumuiya ya kimataifa kujua mbinu ambazo serikali ya Castro inatumia kupata pesa kwa kutumia madaktari wake wanaofanya kazi katika nchi nyingine.

Hii ni “njama ya kupata pesa ambazo ndio njia kuu ya mapato kwa utawala wa Castro,”amesema balozi Kozak.

“Utawala unawaibia madaktari wake kiasi cha asilimia 90 ya mishahara yao - mishahara ambayo madaktaria wanatakiwa wapate, lakini hawajaiona.”Marekani inafanya kazi kuwalinda madaktari wakati inazuia pesa hizi kufikia utawala.

“Nchi ambazo ni wenyeji wa wafanyakazi kutoka Cuba zinastahili kutuma mishahara yao kwenye akaunti zao moja kwa moja badala ya kujaza mifuko ya serikali. Na baadhi ya nchi zimeonyesha kwamba hili linawezekana licha ya pingamizi kutoka kwa utawala,” amesema kaimu waziri Kozak.

“Tunazingatia namna ya kuuzuia utawala wa Castro kupata pesa inazotumia kufadhili utawala wa kibabe nchini Cuba na kuingilia maswala ya Venezuela. Tumefanya hayo kwa kuweka vikwazo maalum kwa jeshi la Cuba, taasisi za usalama na ujasusi,” amesema.

“Tunalenga kuimarisha mashirika ya kijamii ya Cuba, sekta binafsi na wala sio utawala wa kimabavu wa Cuba.”

XS
SM
MD
LG