Accessibility links

Breaking News

Historia Ya Sherehe Za 'Thanksgiving' Marekani


Ifuatayo ni tahariri inayoelezea sera na maoni ya serikali ya Marekani.

Kuna wakati kati ya September 21 na November 11 mwaka 1621, wanaume, wanawake na watoto 53 Waingereza wakiungana na baadhi ya Wamarekani wazawa walishukuru kwa mavuno mazuri ya kwanza na hivyo kuandaa mlo majumbani mwao, katika eneo la Plymouth Colony ambayo hivi leo inajulikana kama Massachusetts.

Walikuwa na mengi ya kushukuru. Mwaka mmoja tu uliopita, katikati ya mwezi November mwaka 1620, walikuwa sehemu ya kundi la Wakoloni 102 na mabaharia 30 ambao walifika katika fukwe za Amerika Kaskazini wakiwa ndani ya meli ya Mayflower. Walikuwa Wapuritan, watu wa dini waliotaka kujitenga ambao walionekana kuwa na msimamo mkali, na hivyo ilikuwa kinyume cha sheria kwa serikali ya Uingereza, nyumbani wanakotokea.

Wakiwa wamechoshwa na mateso huko Ulaya, walielekea katika colony la Virginia. Lakini msimu wa baridi kali sana uliwalazimisha kutia nanga huko Cape Cod, zaidi ya kilometa 350 kaskazini mashariki mwa kituo chao cha awali walicho kichagua.

Hata hivyo, Wakoloni hao waliamua kubakia bara umbali mdogo kutoka kwenye sehemu ambayo walitia nanga huko Cape Copd na kuanza kuunda jamii ambako wangeishi kwa mujibu wa imani zao za dini.

Mwaka wa kwanza ulikuwa mgumu na hivyo walikaribia kuufunga ukoloni wao kabla ya kushika mizizi. Ndani ya mwaka mmoja, karibu nusu ya wakoloni 102 walifariki kutokana na njaa, magonjwa na hali mbaya sana ya hewa. Lakini msimu wa joto ulileta mavuno mazuri, na msimu wa vuli, wanaume 22, wanawake 4, wavulana 9, wasichana 5 na watoto 15 walikaa chini na kushereheka na majirani zao Wampanoag.

Massachusetts haikuwa ya kwanza kudai kwamba jimbo lao lilikuwa la kwanza kusherehekea sikukuu ya Thanskgiving. Nyaraka kadhaa za kihistoria zinaashiria kwamba wasafiri wa Kihispania na Wakoloni wa Kiingereza walisherehekea sherehe za Thanksgiving huko Florida, Texas, Maine na Virginia muda mrefu kabla ya 1620. Hata hivyo, hizi zilikuwa sherehe za kieneo ambazo hazikupitia kipindi kigumu. Kwa hiyo, shukran kwa ushawishi wa nguvu wa jimbo la Massachusetts, Thanksgiving ya kisasa ilipitishwa rasmi katika majimbo yote mwaka 1863 kwa amri ya Rais Abraham Lincoln. Maadhimisho yalihamishiwa wiki ya nne ya mwezi Novemba na Rais Franklin Delano Roosevelt.

Thanksgiving ilianza kwa sala ya shukrani iliyofanywa na wahamiaji ambao kama si kwa msaada wa majirani zao, huenda wasingenusurika katika mwaka wao wa kwanza Amerika Kaskazini.

Hivi leo, ingawaje Thanksgiving kiasili ni mikusanyiko ya familia na marafiki, tishio la maisha na afya linaloletwa na janga la COVID-19 tutaona wengi wakisherehekea nyumbani wakiwa peke yao, kwa mara nyingine tena wakishukuru kwa kupata fursa ya siku njema za usoni.

XS
SM
MD
LG