Accessibility links

Breaking News

Kamanda wa Zamani wa Rwanda Mpiranya Anatafuta Kwa Kushiriki Mauaji Ya Kimbari 1994


Hili ni tangazo la serikali ya Marekani kwa umma.

Protaiy Mpiranya, kamanda wa zamani wa kikosi cha walinzi wa Rais wa Jeshi la Rwanda, anatafutwa kwa kushiriki katika Mauaji ya Kimbari ya 1994 nchini Rwanda.
Aprili 1994, wakati wahutu wenye msimamo mkali wa Rwanda walikuwa wakizindua kampeni ya umwagaji damu ya mauaji ya kikabila, Mpiranya aliongoza Kikosi cha Walinzi wa Rais. Anatuhumiwa kwa jukumu muhimu katika kupanga mauaji ya kimbari, pamoja na kufundisha vikundi vya jeshi na kusambaza silaha

Walinzi wa Rais, chini ya amri ya Mpiranya, wanatuhumiwa kumuua Waziri Mkuu Agathe Uwilin-giyimana na walinda amani kumi wa Ubelgiji waliokuwa kama walinzi wake.

Wakati wote wa mauaji ya kimbari, walinzi wa Rais waliripotiwa kuwa nguvu kubwa ya uasi na uharibifu. Kwa uhalifu huu na mwingine Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Rwanda ilimshtaki Mpiranya kwa mashtaka ya mauaji ya kimbari na uhalifu wa kivita na ikatoa hati za kukamatwa kwake.

Marekani inashirikiana na serikali nyingine, Umoja wa Mataifa na Mahakama ya kimataifa ili iwe ngumu kwa Mpiranya na wengine wanaotafutwa kwa mauaji hayo kuendelea kukwepa haki. Ili kufikia mwisho huo, Marekani inatoa zawadi ya hadi dola milioni tano kwa habari itakayopelekea kukamatwa kwake.

Ikiwa wewe au mtu yeyote unayemjua ana habari za shughuli za Protaiy Mpiranya na mahali alipo, unaweza kuziwasilisha kwa siri. Tafadhali tembelea ubalozi wa karibu wa Marekani au tovuti ya ubalozi kuwasiliana na Ofisi ya Usalama ya Kanda, tuma barua pepe kwa Mpango wa Tuzo za Uhalifu wa Vita vya Marekani katika WCRP@state.gov, au wasiliana nasi kupitia WhatsApp kwa nambari + 1-202-975-5468 au tembelea Ukurasa wa Facebook wa [w w w dot facebook dot com mkwaju war crimes rewards program au tufuate kwenye ukurasa wetu wa Twitter katika [w w w dot twitter dot com mkwaju war crimes rewards] kwa picha za wanaotafutwa.

Ripoti zote za kuaminika zitachunguzwa na utambulisho wa watoa habari wote utafanywa kuwa siri.

XS
SM
MD
LG