Accessibility links

Breaking News

Karne moja ya historia ya wanawake kupiga kura Marekani


Ifuatayo ni tahariri inayoelezea sera na maoni ya serikali ya Marekani. 

Agosti 26, Wamarekani wanasheherekea maadhimisho ya miaka 100 ya kupitishwa sheria ya marekebisho ya 19 ya katiba ya Marekani ambayo inaeleza kwamba “haki ya raia wa Marekani kupiga kura haitakataliwa au kukandamizwa na Marekani au na jimbo lolote katika misingi ya jinsia. Siku hiyo, wanawake Wamarekani milioni 26 walipewa haki ya kusaidia kuamua jinsi nchi yao inavyofanya kazi katika siku zijazo.

Harakati za wanawake kudai haki zilizinduliwa rasmi wakati wa mkutano wa kwanza wa haki za wanawake mwaka 1848. Katika miaka 70 iliyofuata, wagombea wanawake na wanaume walijaribu kila njia inayowezekana kuhalalisha haki ya wanawake ya kupiga kura.

Walizindua mpango wa kupitisha marekebisho ya katiba yanayotoa dhamana kwa haki ya wanawake kupiga kura, mchakato mrefu. Wakati huo huo, baadhi ya wanawake walijaribu kupiga kura kinyume cha sheria na walifungua mashtaka wakati majaribio yao yalipokataliwa, wakitumaini kuwa majaji wangekuwa upande wao.

Hilo liliposhindikana, walifanya kazi kwa kiwango cha serikali ya jimbo, mahala ambapo walifanikiwa zaidi: kufikia wakati marekebisho ya 19 yalipokuwa sheria ya nchi, zaidi ya nusu ya majimbo yote, mengi yakiwa ya huko magharibi, tayari yalikuwa yametoa haki kwa wanawake kupiga kura.

Baada ya utaratibu wa pole pole katika bungeni hapo Juni mwaka 1919, marekebisho ya 19 hatimaye yalipata kura zinazohitajika kupelekwa katika majimbo ili kuidhinishwa kwa robo tatu ya majimbo 48 ya wakati huo. Tennessee ilikuwa jimbo la mwisho lililohitajika kuidhinisha marekebisho ya 19 hapo Agosti 18 mwaka 1920.

Katika hotuba maarufu kutoka mwaka 1873, mmoja wa viongozi wakuu wa kundi la harakati za wanawake, Susan B. Anthony, aliangalia maneno ya ufunguzi kwenye katiba ya Marekani kama kuhalalisha uwezeshaji wanawake: Sisi watu wa Marekani, ili kuunda umoja uliokamilika,kuanzisha haki, kuhakikisha utulivu wa ndani, kutoa utetezi wa Pamoja, kuhamasisha ustawi wa jumla na kupata baraka za uhuru, sisi na kizazi chetu, utnaitunza na kuiweka katiba hii ya Marekani.

“ilikuwa sisi, watu, sio sisi, raia wanaume wa kizungu, wala sisi, raia wa kiume; lakini sisi, watu wote, tuliouunda muungano huu, alisema. “Na tuliuunda sio kutoa baraka za uhuru, lakini kuulinda; sio nusu yetu na nusu ya kizazi chetu, lakini kwa watu wote wanawake pamoja na wanaume”.

Hiyo ilikuwa ni tahariri iliyoelezea sera na maoni ya serikali ya Marekani.

XS
SM
MD
LG