Accessibility links

Breaking News

Maadhimisho ya miaka saba ya shambulizi la kemikali Syria


 Ifuatayo ni tahariri inayoelezea sera na msimamo wa serikali ya Marekani.

Mwezi huu ni maadhimisho ya miaka saba ya shambulizi kali la silaha za kemikali huko Ghouta, Syria. Mnamo Agosti 21, 2013, katika vitongoji vya Damaskus, utawala wa Bashar al-Assad uliwaangamiza zaidi ya Wasyria 1,400, wengi wao wakiwa watoto, kwa kutumia kemikali inayojulikana kama sarin.

Katika kukumbuka waathirika wa unyama huo, Marekani ilitangaza vikwazo sita dhidi ya wanajeshi, serikali, na wafadhili wa serikali ya Assad.

Marekani imeweka vikwazo kwa mfadhili wa Assad, Yasser Ibrahim, chini ya amri ya kiutendaji namba 13894 kwa juhudi zake za kuzuia suluhisho la kisiasa kwa mzozo wa Syria. Kutumia mitandao yake kote Mashariki ya Kati na kwingineko, Ibrahim amesaini mikataba mibovu inayomtajirisha Assad, wakati Wasyria wanakufa kwa ukosefu wa chakula na dawa.

Marekani pia kufuatia agizo hilo la kiutendaji 13894, imeweka vikwazo kwa uongozi katika vitengo kadhaa vya jeshi la Syria kwa juhudi zao za kuzuia kusitisha mapigano nchini humo. Katika Vikosi vya Ulinzi vya Kitaifa Marekani imemteua kamanda Fadi Saqr. Katika Idara ya 4, Kamanda wa 42 wa Brigedi, Brigedia Jenerali Ghaith Dalah pia alitajwa. Mwishowe, katika Vikosi vya Tiger Marekani imemtaja kamanda wa Kikosi cha Haider, Samer Ismail.

Maafisa hawa wakuu wanaongoza jeshi lile lile la Syria ambalo limewaua watoto na mabomu ya kemikali na silaha hizo dhidi ya jamii kama Ghouta, alisema waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo.

"Wamevunja mkataba wa kijamii kati ya raia na wanajeshi walioapa kuwalinda." Tangu Juni 2020, Marekani imewataja zaidi ya watu 55 ambao wameendeleza sera za kikatili za Assad.
Vikwazo hivi vipya vinawakumbusha waathirika wa shambulio la silaha za kemikali za Assad huko Ghouta miaka saba iliyopita, waziri wa mambo ya nje Pompeo aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter. "Hatutaacha kushinikiza uwajibikaji na suluhisho la amani kwa mzozo wa Syria.

XS
SM
MD
LG