Accessibility links

Breaking News

Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa Marekani


Ifuatayo ni tahariri inayoelezea sera na maoni ya serikali ya Marekani.

Wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, Rais Abraham Lincoln amewataka wananchi nchini kwake katika hotuba yake maarufu ya Gettysburg kuhakikisha kwamba uhuru ‘hautapotea kutoka ardhini.” Kwa maneno yamewatia hamasa wengi katika miaka mingi iliyofuata, wakiwemo mamilioni ya wanajeshi katika taifa letu ambao wamepambana kuulinda siyo tu uhuru wa Marekani, lakini ule wa mataifa mengine pia.

November 11 kila mwaka ni siku ya mashujaa, Marekani inachukua muda kuwapa heshima wanaume na wanawake, na thamini za wajibu na kujitoa mhanga walikochukua. Muda mrefu baada ya kuondoka katika jeshi, wamekuwa ni mfano ambao unabainisha maana ya raia kuwa katika ardhi huru.

Sikukuu hii, ambayo huadhimishwa kila mwaka November s11, ilianzia na silaha ambazo zilimaliza vita vya kwanza vya dunia mwaka 1918. Mzozo, ambao ulipiganwa huko Asia, Afrika, na kusambaa kwenye visiwa katika eneo la Pacific na kwenye maji ya Amerika Kusini, pamoja na kwenye uwanja wa mapambano Ulaya, vilionekana kuwa ‘vita vya kumaliza vita vyote.’ Lakini vita vingine vilifuatia, na mwaka 1954 Rais Dwight Eisenhower aliipanua sikuku ya kuwakumbuka wote ambao walihudumu wakiwa katika jeshi katika vita na amani.

Serikali yetu inaendeleza juhudi hizi hadi hivi leo, kwa program za kuwasaidia wanajeshi wa zamani wanaondoka katika jeshi na kutafuta ajira na kuwasaidia kuingia katika maisha ya kiraia.

Katika msingi huu, siku ya mashujaa haihusu vita. Ni kumbukumbu siyo ya ushindi au kushindwa katika uwanja wa mapambano, ni kusherehekea utashi wa maendeleo ya kisiasa na kieneo. Ni siku ya kumbukumbu, kwa siku kama hizo ambazo zinasherehekewa huko Uingereza, Canada, Afrika Kusini na mataifa mengine ambayo yanawapa heshima wanajeshi wa zamani kwa huduma zao na kujitoa mhanga.

XS
SM
MD
LG