Accessibility links

Breaking News

Makubaliano ya kihistoria yafikiwa kati ya Serbia na Kosovo


Ifuatayo ni tahariri inayoelezea sera na msimamo wa serikali ya Marekani

Licha ya mivutano ya kihistoria, Serbia na Kosovo zilichukua hatua za kijasiri kurejesha uhusiano wa kiuchumi. Tarehe 4 Septemba, nchi hizo mbili zilisaini makubaliano yaliosimamiwa na Marekani, zikikamilisha ahadi ya kushirikiana katika masuala kadha ya uchumi.

Wakati wa sherehe za kusaini makubaliano hayo huko White House, rais Donald Trump alisema uamuzi wa rais wa Serbia Aleksandar Vucic na waziri mkuu wa Kosovo Avdullah Hoti kushirikiana pamoja, umefanya kanda hiyo na ulimwengu kuwa salama.

“Baada ya historia ya vurugu mbaya ya mashauriano yaliokwama, uongozi wangu ulipendekeza njia ya kuondoa mgawanyiko.

Kwa kuzingatia ubunifu wa ajira na ukuaji wa uchumi, nchi hizo mbili ziliweza kufikia mafanikio makubwa. Tunajivunia viongozi hawa wakuu na kwa kulifanikisha hili. Na wananchi wao wanawajivunia , labda muhimu zaidi. Ni jambo la kihistoria kabisa.”

Kufuatia kusambaratika kwa Yugoslavia mwanzoni mwa miaka ya 1990 na vita vya Balkan, Kosovo ilijiondoa kutoka Serbia na kutangaza uhuru wake mwaka wa 2008, lakini Serbia ilipinga kutambua uhuru huo wa Kosovo.

Katika kipindi cha miaka 20, juhudi za nchi za magharibi kufanikisha makubaliano kamili ya kisiasa kati ya nchi hizo mbili ziliendelea kukwama. Mjumbe maalumu wa rais Trump kwa Serbia na Kosovo Richard Grennel alisema rais Trump alikuwa amedhamiria kuondoa mvutano huo.

“Alichofanya rais Trump tokea mwanzo kabisa ni kusema: Wacha tuwaonyeshe namna ya kujiendeleza kiuchumi, namna ya kumiliki viwanda na kuvikuza. Wacha tubadili hali hii. Wacha tujue mambo ya uchumi kwanza. Halafu tuone iwapo kujikita kwenye uchumi na kubuni ajira kunaweza kutuliza mzozo wa kisiasa. Hili litaendelea kuonekana.”

Makubaliano ya kufufua ushirikiano wa kiuchumi kati ya Belgrade na Pristina yaliosimamiwa na Marekani, yanalenga kuimarisha ukuaji wa uchumi na kufungua ajira, na kuonyesha faida zinazoonekana za ushirikiano.

Kwa kuongezea, Serbia na Kosovo zinashiriki kwenye harakati zinazoendelea za kusaka amani Mashariki ya Kati. Kosovo na Israel zilikubaliana kuanzisha ushirikiano na kuwa na uhusiano wa kidiplomasia; Serbia ilijikubalisha kuhamisha ubalozi wake mjini Jerusalem, hatua muhimu katika kudumisha ushirikiano kati ya nchi za Ulaya na Mashariki ya Kati.

Kwenye White House, Trump alikiri hisia kali za zamani kati ya Serbia na Kosovo, lakini alitabiri siku njema zijazo.

“Nadhani watakuwa na uhusiano mzuri sana. Na uchumi utawaleta pamoja.”

XS
SM
MD
LG