Accessibility links

Breaking News

Mali Yaunda Serikali ya Mpito Baada ya Mapinduzi


 Ifuatayo ni tahariri inayoeelezea sera na msimamo wa serikali ya Marekani.

Mnamo Agosti 18, Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita alipinduliwa kijeshi katika hatua ambayo ilishutumiwa vikali.

Marekani haraka ilichukua hatua ya kusitisha msaada wake wa kiusalama kwa serikali ya Mali.

Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika magharibi -ECOWAS, ilichukua hatua ya kusitisha uanachama wa Mali katika jumuiya hiyo, na kuiwekea vikwazo hadi serikali ya mpito inayoongozwa na raia itakapo undwa.

Mwishoni mwa mwezi Septemba, Bah N’Daw, ambaye ni afisa wa jeshi mstaafu, katika ngazi ya Kanali, aliteuliwa kuwa raia wa mpito wa Mali.

Kanali Assimi Goita, aliyeongoza mapinduzi, aliteuliwa kuwa makamu wa rais katika serikali ya mpito.

Mwanadiplomasia ambaye ni raia, aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Moctar Ouane, aliteuliwa kuwa waziri mkuu.

Wataiongoza serikali ya mpito kwa muda wa miezi 18 na kuandaa uchaguzi wa kidemokrasia.

Mnamo Oktoba 5, rais wa mpito Bah N’Daw, aliteuwa baraza kamili la mawaziri, na ECOWAS ikaondoa vikwazo ambavyo ilikuwa imeiwekea Mali.

Marekani inaona hatua ya kuundwa kwa serikali ya mpito kama hatua ya kwanza kuelekea katika kurejesha utawala wa kikatiba.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Morgan Ortagus, amesema kwamba Marekani inaisihi serikali ya mpito kuheshimu ahadi yake kwa jumuiya ya uchumi ya nchi za Afrika magharibi ECOWAS, ikiwemo kuandaa uchaguzi wa kidemokrasia katika muda wa miezi 18.

Itakuwa pia muhimu kwa serikali ya mpito kutimiza ahadi zake kwa watu wa Mali, ikiwemo kuimarisha utawala wa nchi hiyo, kupambana na ufisadi, kufanyia mabadiliko sheria za uchaguzi na kutekeleza makubaliano ya mwaka 2015 kuhusu amani na maridhiano nchini Mali.

Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa Kelly Craft amesisitiza kwamba Marekani haitakubali utawala wa kijeshi , kucheleweshwa kwa uchaguzi, au kuandaa uchaguzi ambao sio huru na wazi, akiongezea kwamba uchaguzi huo lazima uwashirikishe kikamilifu wanawake, watu walipoteza makazi na wakimbizi, vijana na makundi ya watu wanaobaguliwa katika sehemu za kaskazini mwa nchi hiyo.

Serikali ya Marekani inawajali sana watu wa Mali, na imetenga kiasi cha dola milioni 54 kwa ajili ya msaada wa kibinadamu kwa watu wa Mali.

Ortagus amesema kwamba Marekani inaamini kwamba Mali iliyostawi kidemokrasia, kimaendeleao na iliyo salama ni muhimu sana kwa kanda nzima ya Sahel.

Kama mshirika wa Mali kwa zaidi ya miaka 60, Marekani itafanya kazi kwa ushirikiano na wale wote watakaochangia kufanikisha malengo hayo.

Sasa ndio wakati wa raia wa Mali kuungana na kujenga taifa lao lililo bora na lenye ustawi kwa wote.

XS
SM
MD
LG