Accessibility links

Breaking News

Marekani kuisaidia Pakistan Kuboresha Usalama Wa Afya Na Ufuatiliaji Wa Magonjwa


Marekani na Pakistan wamebuni juhudi mbili za kuboresha usalama wa afya na ufuatiliaji wa magonjwa nchini Pakistan. Juhudi moja inaelezea uvumbuzi wa njia za kutathmini usalama na ufanisi wa dawa, na nyingine itaongeza uwezo wa nchi kufuatilia kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza.

Mapema Disemba mwaka jana, mamlaka ya udhibiti wa dawa huko Pakistani, kwa kushirikiana na shirika la kimatiafa la maendeleo ya kimataifa-USAID, ilizindua jukwaa lao jipya la la mchakato wa kufuatialia maendeleo na uidhinishaji. Jukwaa hilo linaloitwa mfumo wa usimamizi wa udhibiti taarifa wa Pakistan, litasaidia makampuni ya Pakistan kuomba kwa urahisi vibali vya kutengeneza dawa, pamoja na kuleta dawa salama na zenye kufanya kazi kwenye soko nkwa haraka na katika bei ya gharama nafuu.

Mpango huo pia ulibuniwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya dawa, ikiiruhusu Pakistan kuongeza ushiriki wake katika soko la kimataifa.

Maafisa wa serikali ya Marekani na Pakistan pia walitangaza kuzinduliwa vitengo vya ufuatiliaji wa magonjwa katika wilaya 155, ili kuboresha uwezo wa maafisa wa afya katika eneo kufuatilia kusambaa kwa magonjwa ya kuambukiza, kama vile COVID-19 kote Pakistan.

Taasisi Ya Marekani ya kimataifa ya misaada ya maendeleo -USAID iliunga mkono utoaji mafunzo ya timu za kutoa majibu ya haraka zinazofanya kazi katika vitengo vya ufuatiliaji juu ya namna ya kufuatilia mawasiliano kwa kesi za COVID-19. Timu hizi pia zilifundishwa kutumia takwimu kutambua maeneo yenye uwezekano mkubwa wa COVID-19, ndani ya wilaya, ambapo itaboresha uratibu wa wakati halisi kati ya ngazi za wilaya na majimbo.

Msaidizi maalumu wa waziri mkuu juu ya afya, Dr. Faisal Sultan, alitoa shukrani zake kwa serikali ya Marekani na alikiri kwamba msaada huu utasaidia sana katika kuweka taasisi ya mfumo jumuishi wa uchunguzi wa magonjwa nchini Pakistan.

Marekani na Pakistan zimekuwa mstari wa mbele katika suala hili, sio tu kupitia uongozi wetu wa pamoja katika mipango ya kimataifa kama ajenda ya usalama wa afya ulimwenguni-GHSA, lakini pia katika ngazi ya nchi inafanya kazi kwa karibu na jamii.

Kuwa na uwezo wa kufuatilia kwa haraka, kugundua na kujibu vitisho vya afya ya umma kama vile COVID-19, ni muhimu sana. Ilihamasisha ushirikiano wet una serikali ya Pakistan kuanzisha vitengo hivi vya ufuatiliaji na majibu ya magonjwa ya wilaya na kuwajengea uwezo wafanyakazi takribani 3,000 wa huduma za afya kujibu haraka vitisho vya afya ya umma huko Pakistan, alisema mkurugenzi wa USAID, Julie Koenen.

Tunaishukuru serikali ya Pakistan kwa kuendelea kwa ushirikiano wetu, wakati tunakabiliana na changamoto ya kuunganisha vitengo hivi katika miundo ya majimbo, mikoa na serikali kuu, na hivyo kutoa rasilimali muhimu ili kuzuia kuenea kwa COVID-19 na magonjwa mengine ya kuambukiza.

XS
SM
MD
LG