Program ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ya kutoa tuzo kwa haki, umeahidi zawadi ya mpaka dola millioni 5 kwa yeyote atakaetoa habari ambayo itasaidia kumtambua au kujua mahali alipo Adnan Abu Walid al Sahrawi, ambaye pia anajulikana kama Abu Walid.
Ni mmoja wa viongozi wakuu wa kundi la kigaidi la Islamic State katika eneo kubwa la jangwa la Sahara kwa jina lingine ISIS-GS.
Kundi hilo la kigaidi liliibuka wakati Abu Walid na wafuasi wake waliondoka kwenye tawi la kundi la Al Qaida liitwalo Al Mourabitoun, na kujiunga na kundi hilo.
ISIS GS kimsingi ina makao yake nchini Mali, kwenye eneo la mpaka na nchi ya Niger. Ilitangaza kuungana na ISIS mwezi Mei mwaka wa 2015.
Chini ya uongozi wa Abu Walid, kundi hilo la kigaidi liliendesha mashambulizi kadhaa, likiwemo lile la tarehe 4 Oktoba mwaka 2017, ambapo lilishambulia kikosi cha pamoja cha Marekani na Niger ambacho kilikuwa kinafanya doria karibu na mpaka wa Mali.
Shambulizi hilo lilisababisha vifo vya wanajeshi wanne wa Marekani na wanajeshi wanne wa Niger.
Tarehe 16 Mei mwaka 2018, wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilimtaja Abu Walid miongoni mwa magaidi wakubwa duniani kwa mujibu wa amri ya kiutendaji nambari 13224.
Wakati huo huo, kundi la ISIS -GS lilitajwa kama kundi la kigaidi la kigeni kwa mujibu wa kifungu nambari 219 cha sheria ya uhamiaji na uraia.
Program ya tuzo kwa haki inasimamiwa na idara ya masuala ya diplomasia na usalama ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1984, program hii imekwisha toa zaidi ya dola millioni 150 kwa zaidi ya watu 100 walitoa habari sahihi ambazo zilisaidia kuwakamata magaidi na kuwafikisha mbele ya sheria, au kuzuia vitendo vya ugaidi wa kimataifa kote duniani.
Iwapo kuna yeyote ambae ana habari kuhusu Abu Walid al Sahrawi, anaombwa kuwasiliana na mradi huo wa kutoa zawadi kwenye tovuti ifuatayo: www.rewardsforjustice.net , au aandike barua pepe kwa info@rewardsforjustice.net , au awasiliane na afisa wa usalama wa kikanda kwenye ubalozi wa Marekani au ubalozi mdogo ulio karibu yake.
Habari zote zitahifadhiwa kwa siri.