November 26, mwaka 20098, watu kumi waliokuwa na silaha wenye uhusiano na taaisi ya kigaidi ya kigeni ya Pakistan Lashkar e Tayyiba, walifanya shambulizi kwenye maeneo kadhaa mjini Mumbai nchini India.
Walilenga maeneo ambayo mara kwa mara yalitembelewa na watalii, kituo cha treni na kituo cha jamii ya wayahudi. Shambulizi lilidumu kwa siku kadhaa na mara lilipowksiha, zaidi ya watu 166 kutoka maaifa tofauti walikuwa wameuawa, wakiwemo washambuliaji 9 kati ya 10, na zaidi ya watu 300 walijeruhiwa.
Mshambuliaji aliyenusurika alifariki kwa kunyongwa November mwaka 2012, lakini Sajid Mir, mtu ambaye alipanga shambulizi, alielekeza matayarisho, na kutumkika kama mmoja wa wadhibiti walioko Pakistan wakati wa mashambulizi, na mpaka hivi hajulikani alipo.
Mir alishtakiwa na mahakama ya wilaya ya Kaskazini ya Illinois April 21, mwaka 2011. Mamlaka ilitoa hati ya kukamatwa kwake siku iliyofuata. Mir alishtakiwa kwa njama za kuharibu mali za serikali ya kigeni; kutoa msaada wa vifaa kwa magaidi; kusaidia na kufanikisha kuuawa kwa raia nje ya Marekani; na kupiga mabomu sehemu ambazo zilikuwa zinatumiwa na umma. Mwaka 2019, Mir aliongezwa katika orodha ya FBI ya magaidi wanaotafutwa.
Wizara ya mambo ya nje ya serikali ya Marekani kupitia program ya Rewards for Justice inatoa tuzo ya mpaka dola milioni 5 kwa habari ambazo zitapelekea kukamatwa au kushtakiwa katika nchi yoyote kwa Sajid Mir au mtu yoyote anayehusika na shambulizi.
Sajid Mir alizaliwa ama mwaka 1976 au 1978 mjini Lahore, Pakistan. Ana urefu wa sentimeta 165 au 167 na uzito wa kilo 60. Kwa mujibu wa FBI, Mir ana mabaka usoni mwake, ana kovu. Upande wa shavu la kulia na pia kwenye jicho lake la kulia.
Mtu yeyote ambaye ana habari kuhusu Sajid Mir ni vyema tume ujumbe kwa Rewards for Justice kwa njia ya Whatssapp, Telegram au maandishi katika namba 202 702 7843.
Habari zote zitakuwa siri.