Accessibility links

Breaking News

Marekani na Vietnam zapiga hatua katika kuweka kando tofauti zao


Ifuatayo ni tahariri iliyoeleza msimamo na maoni ya serikali ya Marekani.

Zaidi ya vizazi viwili vilivyopita, Marekani na Vietnam walikuwa vitani. Katika miaka ya 1960 na mwanzoni mwa miaka ya 1970, majeshi ya Marekani yalitumia mamilioni ya galoni za kemikali kuharibu msitu ambao walijificha wanajeshi adui wakati wa harakati zao.

Kemikali ambayo ilijulikana kama Agent Orange, mchanganyiko uliojumuisha dioxin, kemikali ambayo tangu wakati huo tumejifunza imekuwa na athari za kiafya na mazingira .

Tangu vita kumalizika, Marekani na Vietnam wamepiga hatua kubwa katika kuweka kando tofauti zao, mwishowe kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia mnamo mwaka 1995.

Nchi hizi mbili sasa zinashirikiana kwa kiasi kikubwa katika biashara na uhusiano wa kiuchumi. Wanashirikiana katika nyanja za sayansi na teknolojia, elimu, mazingira na afya, ulinzi na usalama, na kutatua maswala ya urithi wa vita.

Ushirikiano juu ya urekebishaji wa mazingira, au kusafisha maeneo ambayo yalikuwa yamechafuliwa sana na kemikali iitwayo Agent Orange, yalikuwa juu kwenye orodha.

Kwa ombi la Serikali ya Vietnam, Serikali ya Marekani, ilifanya kazi kupitia Shirika la Kimataifa la Misaada ya Maendeleo USAID, ilikubali kukamilisha kusafisha Uwanja wa ndege wa Đà Nẵng, ambao ulikuwa na viwango vya juu vya dioksini kwenye mchanga uliosalia kutoka kwenye vita. Mradi huo ulikamilishwa mwaka 2018.

Kilichofuata kwenye orodha hiyo ilikuwa eneo la uwanja wa ndege wa kijeshi wa Biên Hòa eneo ambalo lilihifadhi na kutunza kemikali ya Orange wakati wa Vita vya Marekani na Vietnam na eneo kubwa zaidi la kemikali ya dioxin huko Vietnam.

USAID inakadiria juhudi za jumla za kurekebisha zitakamilika kwa kipindi cha miaka kumi. Mwishoni mwa Novemba mwaka huu, Mshauri wa Usalama wa Kitaifa Robert O'Brien alitangaza kuwa USAID itachangia dola nyingine milioni 20 kusafisha eneo la uwanja wa ndege wa kijeshi wa Biên Hòa na kufikisha jumla ya mchango wa Marekani kuwa zaidi ya dola milioni 110.

Zamani, tulikuwa wapinzani kwenye uwanja wa vita. Lakini leo, uhusiano wetu wa usalama unahusu ushirikiano, "Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alisema.

"Tangu wakati huo, tumejenga urafiki juu ya maslahi ya kawaida, kuheshimiana, na dhamira ya ujasiri ya kuachana na yaliyopita na kutazama siku zijazo.

Marekani imejitolea kufanya kazi na Serikali ya Vietnam kusuluhisha madhila ya urithi wa kivita wakati ikiendelea kuimarisha uhusiano wa kiuchumi, kitamaduni, na usalama kati ya nchi hizo mbili.

Jitihada za USAID kusafisha dioksin kote Biên Hòa na Đà Nẵng zimekuwa muhimu katika kujenga uaminifu na ushirikiano wakati wa kuimarisha Uhusiano mkubwa wa Marekani na Vietnam.

XS
SM
MD
LG