Accessibility links

Breaking News

Marekani : Siku Ya Kumuenzi Martin Luther King, Jr


Ifuatayo ni tahariri inayoelezea sera na maoni ya serikali ya Marekani. 

Jumatatu ya tatu ya mwezi Januari, tunatoa heshima ya kumbukumbu ya Martin Luther King Jr. Mchungaji wa kanisa la Baptist kutoka jimbo la kusini la Alabama, Dr.King alikuwa kiongozi katika harakati za haki za kiraia nchini Marekani, ambaye alitetea mabadiliko ya kijamii kupitia njia zisizo za vurugu.

Mafanikio makubwa ya Dr.King yalikuja kwa kupitishwa sheria ya haki za kiraia mwaka 1964, ambayo ilipiga marufuku ubaguzi katika ajira na ubaguzi katika maeneo ya umma, na sheria ya haki ya kupiga kura yam waka 1965. Ushindi huu wa vitu viwili ulikuwa na matokeo makubwa, sio tu kwa Marekani, lakini kote Duniani.

Mapambano ya Dr.King dhidi ya udhalimu wa rangi hayakupanuka kuhamasisha usawa wa rangi kupitia sheria ya kimataifa. Japokuwa maneno na vitendo vyake vilitumika kama msukumo kwa darzeni ya wanaume na wanawake kote duniani ambao walitaabika dhidi ya ukoloni, ubaguzi wa rangi na ukosefu wa haki za llinapokuja suala la rangi.

Enzi za baada ya vita vya pili vya Dunia zilitofautishwa na ukoloni kote ulimwenguni. Nchi mpya ziliibuka kutoka makoloni ya zamani, na kati ya mwaka 1945 na mwanzoni mwa miaka ya 1960, uanachama katika Umoja wa Mataifa uliongezeka zaidi ya mara mbili hadi kufikia 115. Takribani asilimia 75 ya wanachama wapya walikuwa nchi zinazoendelea ambazo idadi ya watu wao mara nyingi walikuwa wakiteseka, chini ya sheria za kibaguzi na vitendo visivyo vya haki.

Wawakilishi wengi wa mataifa haya mapya walivutiwa na kampeni ya Dr. King ya upinzani kwa njia ya amani na matokeo yake ya moja kwa moja ya kupitishwa kwa sheria ya haki za kiraia. Inashangaza kidogo wakati huo, kwamba vipaumbele vyao vilikuwa tofauti sana kutoka vile vya Dunia ilioendelea, na walichukua mapambano yao kwenye Umoja wa Mataifa, jukwaa kuu la utatuzi wa mizozo kwa amani. Ujumbe wao ulikuwa na idadi, na kwa hivyo walipanga mijadala, na waliungana katika harakati zao za kupambana na dhuluma za rangi.

Matokeo Yake yalikuwa kupitishwa mwaka 1965 kwa mkataba wa kimataifa juu ya kutokomeza aina zote za ubaguzi. Mwaka uliofuata, UN ilipitisha mkataba wa kimataifa juu ya haki za kiraia na kisiasa, na mkataba wa kimataifa juu ya haki za kiuchumi na kijamii, ukichukuliwa kuwa mikataba miwili muhimu kabisa ya haki za binadamu, tangu azimio la ulimwengu la haki za binadamu mwaka 1948.

Kote duniani, kama vile homa, harakati za uhuru zinasambaa katika ukombozi mkubwa sana katika historia. Umati mkubwa wa watu waliazimia kumaliza unyonyaji wa rangi na ardhi yao, alisema Dr.King katika hotuba yake ya kukubali tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1964, moja ya mara chache alipohutubia kuhusu mapambano ya ulimwengu kwa usawa wa rangi.

Tunachokiona hivi sasa ni mlipuko wa uhuru.

XS
SM
MD
LG