Accessibility links

Breaking News

Marekani Yaadhimisha Siku ya Kumbukumbu ya Columbus


Ifwatayo ni tahariri inayoelezea sera na msimamo wa serekali ya Marekani.

Oktoba 12 mwaka wa 1492, meli tatu za Hispania zikiongozwa na Christopher Columbus, ziliwasili kwenye kisiwa ambacho hivi leo kinajulikana kama Bahamas.

Kumbukumbu ya tukio hilo ambayo inaadhimishwa kila mwaka nchini marekani kama siku ya Columbus, ilianzisha mabadilishano makubwa ya chakula, wanyama, mimea, watu na magonjwa ambayo yaliubadilisha ulimwengu unaojulikana leo kama Columbia Exchange.

Kwa sababu hiyo, mwaka 1492 unachukuliwa na wanahistoria wengi, kama mwaka muhimu zaidi katika historia ya ulimwengu wa kisasa.

Idadi ya watu ulimwenguni iliongezeka kwa zaidi ya mara nne tangu mwaka wa 1492, na kuongezeka maradufu kati ya 1650 na 1850.

Licha ya kuwa vigezo vingi kuchangia kwenye ongezeko hili kubwa la ukuaji, ni dhahiri lililo muhimu zaidi ni ongezeko na kuboreka kwa ugavi wa chakula. Ukiongezea pia ugawaji chakula cha mimea ya asili ya marekani kama mahindi, viazi, nyanya, karanga, muhogo, nanasi, pilipili na mbegu za kakao, ilikua jambo muhimu zaidi.

Viazi ilikua chanzano kikuu cha chakula kwa watu maskini katikati na kaskazini mwa bara la ulaya. Mahindi na muhogo vililetwa barani Afrika katika karne ya 16 na kuchukua nafasi ya mazao ya asili ya kiafrika na kuwa chakula kikuu muhimu sana barani humo.

Mazao mapya ya chakula yaliopelekwa china hasa viazi, mahindi na karanga, yalisababisha ongezeko kubwa la watu nchini humo kati ya miaka ya 1500 na 1650. Katika karne ya 18, zaidi ya thulithi moja ya raia wa ulimwengu walikua wanaishi china.

Columbian Exchange iligeuka siku ya kimataifa, vyakula vipya vilitangazwa kila kona ya dunia. Kabla ya mwaka 1492, hapakuwepo machungwa huko Florida, hapakuepo ndizi nchini Ecuador wala pili pili hoho huko nchini Hungary.

Mabadilishano yalipeleka nyanya nchini Italy, kahawa nchini Colombia na Indonesia, nanasi visiwani Hawaii, miti ya mpira ilipelekwa barani Afrika, pilipili ilipelekwa Thailand, China na India, na chokoleti nchini Uswiss.

Kuwasili kwa meli hizo 3 ndogo kwenye kisiwa cha Bahamas kulileta mabadiliko yasiokua ya kawaida katika historia. Iliunda mustakabali wa binadamu kwa karne zirjazo, sio tu kwa sababu ya kupatikana bara jipya, lakini kwa sababu ilileta mawasiliano ya mara kwa mara kati ya maeneo tofauti ya dunia, ikianzisha biashara, ikiruhusu kubadilishana fikra, na kuunda uhusiano na kukutana kati ya tamaduni.

Mwaka wa 1492, watu wa ulimwengu walianza kuungana pamoja kama jamii ya ulimwengu.

XS
SM
MD
LG