Accessibility links

Breaking News

Marekani Yaendelea Kuzisukuma Propaganda Za Kikomunisti


Ifuatayo ni tahariri inayoelezea sera na maoni ya serikali ya Marekani.

Marekani inaendelea kuzisukuma propaganda za kikomunisti za wachina. Hivi karibuni, wizara ya mambo ya nje ilizitaja operesheni za Marekani kwa makampuni sita ya habari yenye makao yake nchini China kuwa ni taasisi za nje, amesema waziri mambo ya nje Mike Pompeo.

“Yote hayo kimsingi yanamilikiwa au kudhibitiwa na serikali ya kigeni. Sisi tunachotaka ni kuhakikisha kwamba watu wa Marekani, wateja wa habari, wanaweza kutofautisha kati ya habari zilizoandikwa na uhuru wa habari na propaganda ambazo zinatawanywa na chama cha kikomunisti cha China. Hayo si jambo moja.”

Taasisi hizi sita zimetajwa chini ya sheria ya Taasisi za Kigeni ikiwemo Yicai global, Jiefang Daily, Xinmin Evening News, Social Sciences katika China Press, Beijing review, na Economic Daily kuwa ni taasisi za kigeni.

Katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja uliopita, hasa chini ya utawala wa katibu mkuu Xi Jinping, chama cha kikomunisti cha China au CCP, kimekuwa na udhibiti mkubwa sana juu ya vyombo vya propaganga ambavyo vinasimamiwa na serikali ya China.

Katibu Mkuu Xi mwenyewe alieleza, “vyombo vya habari ambavyo vinamilikiwa na chama, vinakumbatia nia, vinalinda mamlaka ya chama, hatua zao lazima ziwe na uthabiti mkubwa kwa chama.” Wakati vyombo huru kote duniani vinanagalia ukweli, vyombo vya habari vya PRC vinaiangalia CCP, amesema msemaji wa wizara ya mambo ya nje Morgan Ortagus katika taarifa yake.

Uamuzi wa kuzitaja taasisi hizi sita hauweki masharti yeyote kwa kile ambacho taasisi hizi huenda zitachapisha kazi zake nchini Marekani. Kwa urahisi wanazitamba kwa vile ambavyo walivyo ni taasisi za propaganda zinazodhibitiwa na PRC.

Hatua hii inafuatia kutajwa hapo June 22 Kituo kikuu cha televisheni cha China, Shirika la Habari la China, People’s Daily, na Global Times na hapo Februari 18 iliyataja shirika la habari la Xinhua, China Global Television Network, China Radio International, China Daily Distribution Corporation na Hai Tian Development USA.

Vyombo ambavyo vimetjwa kama taasisi za kigeni lazima viheshimu aina fulani ya mahitaji ambayo yanaongeza uwazi kuhusiana na kujihusisha kwao na harakati za serikali za habari hapa nchini Marekani.

“Lengo letuni kulinda uhuru wa habari hapa Marekani, na kuhakikisha kuwa watu wa Marekani wanafahamu iwapo habari zao zinatoka kwenye vyombo huru vya habari au serikali mbaya ya kigeni,” amesemasmemaji wa Ortagus. “Uwazi hauwatishi wale ambao wanathamini ukweli.”

XS
SM
MD
LG