Hatua ya Marekani kusimamia haki za binadamu ndani ya nchi, imethibitika kuwa ni mwangaza wa matumaini kwa wanaume na wanawake walio nje wanaotafuta uhuru wao.
Ripoti ya hivi karibuni ya tume iliyoangazia kupatikana kwa haki za binadamu, imesisitiza umuhimu wa viongozi wa Marekani kusimamia haki za binadamu kama kanuni za msingi za sera ya Marekani ya mambo ya nje, amesema Peter Berkowitz, mkurugenzi wa mipango ya sera katika wizara ya mambo ya nje.
“Kwa uchache ni muhimu kwa viongozi wetu kuzungumzia kwa nguvu kuhusu misingi ya Marekani ambayo imeelezwa katika tangazo la uhuru wa Marekani, iliyotokana na muundo wa serikali ya Marekani ambapo nguvu zote halali za kisiasa zinatokana na ridhaa za wale wanaotawaliwa. Na madhumuni ya kwanza ya serikali ni kuhakikisha haki zinapatikana kwa watu wote. Kuonyesha hilo ni sehemu muhimu kwa sera ya mambo ya nje ya Marekani.”
Ripoti ya tume pia imegundua kwamba Marekani inaweza kuwa na ufanisi mkubwa katika kuhamasisha haki za binadamu nje ya nchi, wakati ambapo inalinda haki hizo nyumbani, amesema bwana Berkowitz.
Na mwisho, haki za binadamu lazima zihusishwe katika jamii, ili ziwe na nguvu katika utamaduni wa siasa, amesema mkurugenzi Berkowitz.
“Kulindwa kwa haki za binadamu, kuhamasisha haki za binadamu, hizi si hatua zinazoweza kuja zenyewe tu. Zinapaswa kushughulikiwa. Namna gani zinaweza kushughulikiwa, ni kuheshimu haki za binadamu? Zikuzwe katika ngazi ya familia, jamii, mifumo ya elimu, kwenye utamaduni wa siasa katika namna ambayo raia watakuwa na uelewa nazo, ambazo zinawafundisha namna ya kuheshimu haki ambazo zinasimamiwa na kila mtu.”
Katika kuhamasisha mafanikio ya haki za binadamu nje ya nchi, ameeleza mkurugenzi Berkowitz, ni muhimu kulenga siyo tu kwenye tangazo la uhuru, lakini pia katika azimio la ulimwengu kuhusu haki za binadamu, ili kutafuta kiini kidogo ambacho ni muhimu kwa haki ambacho kinaweza kutumika kama kigezo popote pale katika siasa.