Kulingana na Mtandao wa Mifumo ya Maonyo ya Mapema ya Njaa, au FEWS NET, inayosimamiwa na USAID, Sudan Kusini imejikuta katika mgogoro mwingine mkubwa. Ukubwa na ukali wa ukosefu mkubwa wa usalama wa chakula nchini Sudan Kusini hadi Januari 2021 utabaki kuwa wa rekodi ya juu kabisa tangu 2014.
Hali mbaya ya hewa na kuyumba kwa uchumi ni sehemu ya tatizo, lakini pia na mzozo mbaya.
Kulingana na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani -WFP mafuriko yalisambaa kabla tu ya kipindi cha mavuno ya kila mwaka, yameosha mashamba na kuua mifugo, ikizidisha hali ambayo tayari ni tete, na kusababisha njaa, utapiamlo, na ukosefu wa makazi. Watoto walio chini ya umri wa miaka 5 wameathirika sana.
Wakati huo huo, janga la COVID-19 na hatua muhimu za kuzuia zinaongeza tayari hali ambayo ni mbaya ya kibinadamu na inadhoofisha mfumo dhaifu wa huduma za afya. Matokeo, yake karibu watu milioni 7.5 sasa wanahitaji misaada ya kibinadamu huko Sudan Kusini.
Mnamo Septemba 24, Marekani ilitangaza karibu dola milioni 108 kwa ajili ya misaada ya kibinadamu kwa watu wa Sudani Kusini, ikiwa ni pamoja na wale raia wa Sudan Kusini walio katika nchi jirani, kwenye hafla ya kiwango cha juu wakati wa Mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa mataifa. Mazungumzo na Wafadhili kumi wa juu duniani juu ya Mahitaji ya Kibinadamu Ulimwenguni.
Misaada ya kibinadamu ya Marekani inatoa msaada wa dharura wa chakula, huduma za afya, upatikanaji wa maji salama ya kunywa na usafi wa mazingira, na msaada kwa waathirika wa manyanyaso ya kijinsia nchini Sudan Kusini, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alisema katika taarifa ya maandishi.
Misaada ya kibinadamu ya Marekani pia inatoa shughuli za kuokoa maisha kwa wakimbizi karibu milioni 2.2 wa Sudan Kusini katika nchi jirani, ambao wengi wao ni wanawake na watoto, na kwa jamii za wenyeji zinazohifadhi wakimbizi.
Marekani pia inatoa msaada kwa Huduma ya usafiri wa anga ili kusafrisha wafanyakazi wa huduma za kibinadam wa Umoja wa Mataifa na vifaa vya misaada kote Sudan, na pia shughuli za mtandao wa mashirika karibu 30 yasiyo ya kiserikali.
Marekami inabaki kuwa mfadhili mkuu zaidi wa misaada ya kibinadamu, kote Sudan Kusini na ulimwenguni, alisema waziri wa mambo ya nje Pompeo. Tutaendelea kuwa kichocheo cha mwitikio wa kimataifa wa kupunguza mateso ya watu wa Sudan Kusini.
Tunashukuru michango kutoka kwa wafadhili hadi leo lakini tunatambua mahitaji muhimu ambayo yamebaki na tunatoa wito kwa wafadhili wa sasa na wapya kutoa michango mipya au kutimiza ahadi zilizopo ili kufanikisha msaada huu wa kuokoa maisha.