Accessibility links

Breaking News

Marekani Yaiwekea Vikwazo Serikali ya Uturuki na Urais wa Viwanda Vya Ulinzi


Ifuatayo ni tahariri inayoeleza msimamo na maoni ya serikali ya Marekani.

Marekani inaweka vikwazo kwa serikali ya Uturuki na urais wa Viwanda vya Ulinzi kwa kununua mfumo wa ulinzi wa makombora aina S-400 kutoka Rosoboron , kitengo kikuu cha Russia cha usafirishaji wa silaha.

Vikwazo hivyo ni pamoja na marufuku kwa leseni zote mpya za Marekani za usafirishaji na idhini kwa SSB, na kufungia mali na vizuizi vya viza kwa Dkt Ismail Demir, rais wa SSB, na maafisa wengine watatu wa SSB.

Vikwazo hivi havina nia ya kudhoofisha uwezo wa kijeshi au utayari wa Uturuki au mshirika mwingine wa Marekani . Badala yake, vimekusudiwa kuweka gharama kwa Russia kutokana na harakati zake nyingi na mbaya.

U.S. SANCTIONS TURKEY’S PRESIDENCY OF DEFENSE INDUSTRIES

Marekani iliweka wazi kwa Uturuki kuwa ununuzi wake wa mfumo wa makombora ya S-400 utahatarisha usalama wa teknolojia ya jeshi la Marekani na wafanyakazi na kutoa fedha nyingi kwa sekta ya ulinzi ya Russia , na pia kufika kwa Russia kwenye vikosi vya kijeshi la Uturuki na sekta ya ulinzi.

Uturuki iliendelea mbele na ununuzi na majaribio ya makombora ya S-400, licha ya kupatikana kwa mifumo inayoweza kushirikiana ya NATO kukidhi mahitaji yake ya ulinzi. Uamuzi huu ulisababisha kusimamishwa kwa Uturuki na kusubiri kuondolewa kutoka kwenye ushirikiano wa kimataifa wa F-35 Pamoja na Ushirikiano wa Strike Fighter.

Vikwazo hivi vinatoa ishara wazi kwamba Marekani haitavumilia shughuli muhimu na sekta za ulinzi na ujasusi za Russia.

Katika taarifa iliyoandikwa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo aliisihi Uturuki kutatua shida ya S-400 mara moja kwa kushirikiana na Marekani.

Uturuki ni mshirika wa kuthaminiwa na mshirika muhimu wa kanda wa usalama kwa Marekani na tunataka kuendelea na historia yetu ya miaka mingi ya ushirikiano wenye mafanikio wa sekta ya ulinzi kwa kuondoa kikwazo cha umiliki wa Uturuki wa makombora ya S-400 haraka iwezekanavyo.

XS
SM
MD
LG