Accessibility links

Breaking News

Marekani Yakiwekea Vikwazo Kikosi Cha Qods Cha Iran


Ifuatayo ni tahariri inayoelezea mtizamo na maoni ya serikali ya Marekani.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mzozo wa kibinadamu nchini Yemen ni mbaya sana hapa duniani. Yemen tayari ilikuwa nchi maskini kabla ya mzozo kusambaa mwaka 2015, lakini kuendelea kwa mapigano kati ya wahouthi, wakisaidiwa na Iran, na majeshi ya serikali inayotambuliwa kimataifa yamesababisha kusambaa kwa uharibifu.

Kama Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo alivyosema katika taarifa yake, “uungaji mkono wa Iran kwa Wahouthi unachochea mzozo nchini Yemen na kueneza hali ya ukosefu wa uthabiti nchini.” Uungaji mkono huo unaongozwa na kikosi cha ulinzi cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Qods Force, IRGC QF ambacho ni kitengo muhimu cha utawala wa Iran lengo kuu likiwa ni kutekeleza sera za kuunga mkono makundi ya kigaidi na waasi.

Disemba 8, Marekani ilimtaja Hassan Irlu, afisa wa IRGC-QF, ambaye hivi karibuni Iran ilimpeleka San’aa kama balozi wa utawala huo kwa waasi wa Kihouthi.

Kama Wizara ya Fedha ya Marekani ilivyoelezea katika taarifa, “Iran ni taifa pekee kutambua rasmi, na kuteua mwakilishi rasmi kwa wa Houthi. Kwa miaka kadhaa, Irlu ameunga mkono juhudi za IRGC-QF kutoa silaha za hali ya juu na mafunzo kwa wahouthi. Irlu ameendeleza uhusiano uliokuwepo na kamanda wa zamani Qasem Soleimani. Pia ametoa mafunzo kwa wanachama wa Hezbollah nchini Iran.”

Waziri Pompeo alitangaza kwamba kwa “kumpeleka Irlu Yemen, IGRC-QF inaashiria azma yake ya kuongeza msaada kwa wahouthi na kuzidi kukanganya juhudi zaidi za kimataifa kuweza kufikia suluhisho. Marekani,” amesema “inaendelea kuunga mmongo juhudi, kufakinikisha sitisho la mapigano na suluhisho la kisiasa.”

Disemba 8, Marekani pia iliitaja chuo kikuu cha kimataifa la Al Mustafa chenye makao yake nchini Iran kwa kufanikisha juhudi uandikishaji za IGRC QF katika matawi yake mengi ya kimataifa. Yousef Ali Mufaj raia wa Pakistan, ambaye amehusika katika juhudi za IGRC-QF kupanga na kutekeleza operesheni huko Mashariki ya Kati naye pia amekewa vikwazo na Marekani.

“IGRC-QF inachukua fursa ya kila nafasi kusukuma mbele ajenda zake za ghasia na uharibifu, ikiwemo kutumia mizozo kote katika Mashariki ya Kati na kuwalazimisha watu walio katika mazingira hatarishi kupigana kwa niaba ya utawala wa Iran,” amesema waziri Pompeo. “Marekani itaendelea kutumia nyenzo zilizopo kuzionyesha na kukabiliana na tabia hii mbaya.”

XS
SM
MD
LG