Accessibility links

Breaking News

Marekani Yasisitiza Itaendelea Kusimamia Utekelezwaji Wa Haki Za Kimataifa


Ifuatayo ni tahariri inayoeleza sera na msimamo wa serikali ya Marekani.

Marekani ina nia ya dhati kusimamia utekelezwaji wa haki za kimataifa. Jambo la kipekee kati ya wizara za mambo ya nje duniani . Wizara ya Mambo ya Nje Marekani ina ofisi maalum iliyojitolea kushughulikia ukatili mwingi, kama Balozi Morse Tan, anayeongoza Ofisi ya Haki ya sheria ya Jinai Ulimwenguni, alisema katika mahojiano ya hivi karibuni:

Tunazungumzia kuhusu mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu, na chochote tunachoweza kufanya kusaidia kuzuia, kupunguza au kushughulikia dhuluma za aina hii, dhuluma hizi mbaya,. Hayo ndiyo tunayofanya.

Balozi Tan alisema ofisi yake inamshauri waziri wa mambo ya nje wa Marekani na inasaidia kupata rasilimali nyingi za serikali ya Marekani juu ya maswala yanayohusiana na haki za jinai ulimwenguni.

Iwe ni ya kiuchumi, iwe ya kidiplomasia, iwe ni halali, iwe ni ya kijeshi. Kuna safu nzima ya nyanzo tofauti ambazo serikali ya Marekani inazo. Na sisi unaweza kusema s ni kama duka la sera.

Balozi Tan alisema Ofisi ya Haki ya Jinai Ulimwenguni inashirikiana ujumbe huo wa kimsingi na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kuwafikisha waliohusika na unyanyasaji wa haki mbele ya sheria. Lakini kwa sababu ya maswala ya uhuru wa nchi , Marekani haijawahi kuwa sehemu ya Mkataba wa Roma uliounda ICC. Na kwa bahati mbaya, ICC imegeuka kutoka kwa mwelekeo wake kama korti ya uamuzi wa mwisho iliyoundwa kuchunguza na kushtaki uhalifu mbaya zaidi wa kimataifa badala yake, Balozi Tan anasema , ICC imekuwa ya siasa na ufisadi.

Ni Marekani , alisema, ambayo inaendelea kuongoza ulimwenguni katika kutekeleza uwajibikaji kwa uhalifu mkubwa.

ICC haiko pekee mjini katika misingi ya korti za kimataifa, au mahakama za mseto ambazo sehemu fulani ni za ndani na sehemu za kimataifa, na pia mahakama za ndani. Na hiyo ni kweli kwa Korti Maalum ya Lebanoni, ya Kosovo, IIIM, ambayo inajaribu kukusanya habari juu ya ukatili uliofanywa huko Syria, au IIMM, ambayo imejaribu kukusanya ushahidi kuhusiana na unyama uliofanywa huko Myanmar. Tunaunga mkono haya yote, na pia tunasaidia katika suala la ukusanyaji wa ushahidi.

Balozi Tan alisema Marekani ina nia ya dhati kabisa na imedhamiria katika harakati zake za haki ya ulimwengu.Kufikiria juu ya wale ambao wameteseka kutokana na ukatili huu mkubwa kuwapa motisha kubwa, alisema na ikiwa kuna chochote, tunapanua na kuongeza rasilimali zetu katika kutekeleza jukumu hili.


XS
SM
MD
LG