Accessibility links

Breaking News

Marekani Yaweka Vikwazo Dhidi Ya Majeshi Ya Syria, Taasisi na Watu 19


Picha za watu waliofariki na kujeruhiwa za wanaume, wanawake na watoto mjini Douma nchini Syria baada ya serikali ya Assad ikiungwa mkono na Iran na Russia kushambulia kwa risasi kwenye mji huo katika eneo lenye harakati nyingi la sokoni mwaka 2015 zinavunja moyo.

Takriban watu 70 waliuwawa na zaidi ya 500 kujeruhiwa kwenye shambulizi hilo la Oktoba 30. Picha hizo zinaibua kumbukumbu za gharama kubwa ya vita vya Bashar al Assad dhidi ya watu Syria ambavyo vimeuwa zaidi ya watu nusu milioni katika kipindi cha miaka Tisa na nusu iliopita.

Novemba 9 wakati wa kumbukumbu ya waathirika wa mauaji ya Douma pamoja na ukatili mwingine uliotendwa na utawala wa Assad, Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na ile ya fedha ya Marekani imewawekea vikwazo watu 19 pamoja na taasisi chini ya sheria ya Caesar Syrian Civilian Protection ya mwaka 2019.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani pia imeweka vikwazo kwa majeshi ya kitaifa yenye uhusiano na Assad pamoja na kamanda wake mmoja Saqr Rostrom kutokana na juhudi za kuingilia kati sitisho la mapigano nchini Syria.

Wizara ya Fedha ya Marekani kitengo kinacho dhibiti uwekezaji wa nje cha OFAC tayari kimechukua hatua dhidi ya maafisa wa jeshi la Syria, wabunge, maafisa wa ngazi za juu kwenye serikali ya Syria pamoja na Walebanon wanaojaribu kufufua sekta ya mafuta ya Assad.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo alikuwa na haya ya kusema. “Vikwazo viivyowekwa na serikali ya Marekani vinaashiria namna serikali ya Assad ilivyoharibu taasisi za serikali” Waziri wa Fedha Steven Mnuchin pia alisisitiza kwamba wizara yake itaendelea kuweka vikwazo vya kiuchumi dhidi ya utawala wa Assad pamoja na washirika wake.

Wale pia wanaofanya biashara na watu binafsi 19 na taasisi zilizotajwa wanahatarisha kuwekewa vikwazo dhidi yao pia. Pompeo amesema kuwa vikwazo walivyo weka havilengi mashirika na taasisi za kutoa misaada na kwamba Serikali ya Marekani itaendelea kutoa misaada kwa watu wa Syria.

Pompeo pia ameongeza kusema kuwa serikali ya Marekani inajitahidi kuona watu wa Syria wakipata jawabu la kupata suluhisho la kudumu kwa mzozo wa kisiasa kulingana na azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa nambari 2254.

Mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa kwa ajili ya Syria Geir Pedersen ametoa wito wa sitisho la mapigano nchi nzima, kuwachiliwa kwa wafungwa wa kivita , kuandikwa kwa katiba mpya pamoja na kuitishwa kwa uchaguzi utakaosimamiwa na Umoja wa Mataifa.


Waziri Pompeo amesema kuwa utawala wa Assad una chaguo la kuleta suluhisho la kudumu la mapigano yaliodumu kwa karibu muongo mmoja au kuendelea kuwekewa vikwazo zaidi.

XS
SM
MD
LG