Accessibility links

Breaking News

Ripoti Za Kustusha Juu Ya Ajira Za Watoto Katika Uvuvi


Ifuatayo ni tahariri inayoelezea sera na maoni ya serikali ya Marekani.

Katika miaka michache iliyopita, mahitaji ya dunia ya bidhaa za chakula za baharini yamepita idadi ya ukuwaji wa idadi ya watu. Matokeo yake uvuvi umeongezeka zaidi, hasa katika himaya za maji yanayofikika kiurahisi.

Kutokana na hilo kiwango cha samaki kimepungua, wavuvi lazima waende mbali sana baharini ili kuvua. Safari kama hizo zinaongeza gharama ya vitu kama mafuta na nguvu kazi, na wale wanaofanyakazi bila uangalizi wanajiingiza katika njia za kihalifu ili kuongeza faida.

Moja ya eneo linalotumiwa katika kupunguza gharama ni utegemezi wa kufanyishwa kazi kwa nguvu. “Sekta ya uvuvi inaleta tishio kubwa katika usafirishaji watu kihalifu,” inaeleza ripoti mpya ya Usafirishaji Watu katika maeneo ya uzalishaji wa chakula kutoka baharini, ambayo imewasilishea kwa pamoja katika bunge la Marekani na wizara ya mambo ya nje, na idara ya taifa ya usimamizi wa bahari na Atomic ama NOAA. “Kazi za namna hiyo zinaelezwa kuwa ni hatari, na mara nyingi zinategemea sana wafanyakazi wasio na ujuzi, wahamiaji, na vibarua, na wale walio katika mazingira hatari ya kusafirishwa kinyume cha sheria.”

Vitendo hivyo vya kihalifu ni rahisi kufichwa kwa sababu uvuvi kwa asili yake ni kazi inayojitenga. Meli za uvuvi wakati mwingine zinatumia miezi, ama hata miaka kadhaa baharini. Hii inafanya kuwa ni jambo karibu lisilowezekana kwa wavuvi wanao lazimishwa kufanyakazi kukimbia, ama kuripoti vitendo vibaya. Waathirika wa usafirishaji watu mara nyingi hukumbwa na manyanyaso ya kimawazo na hata udhalilishaji wa moja kwa moja, ambao mara nyingine unasababisha vifo, muda mrefu wa kufanyakazi, mazingira mabaya ya kuishi na kulipwa kwa kiwango cha chini, ama kutolipwa kabisa.

Matumizi ya ulazimishwaji wa watu kufanyakazi katika sekta ya uvuvi pia yanaweza kutokea katika mataifa yasiyo na uthabiti wa kisiasa ambayo yana uangalizi mdogo wa kisheria kwa ustawi wa wafanyakazi na uthamini wa utu wao, haki, na uangalizi katika vitendo vya hali ya juu vya rushwa, uhalifu, ghasia, na umasikini. Ripoti hata hivyo inapendekeza kwamba Marekani inatekeleza hatua nne kuelekea kuondoa hali hii. Kwanza Marekani lazima ianzishe majibu ya serikali kwa ujumla katika kukabiliana na usafirishaji wa watu katika uzalishaji wa vyakula kutoka baharini, kote ndani na kimataifa.

Pili, Marekani lazima ihamasishe, na kusaidia juhudi za kukabiliana na usafirishaji watu katika mataifa yanayofahamika kuwa na matatizo na ulazimishaji watu kufanyakazi katika sekta ya uvuvi.

Tatu Marekani lazima ihamasishe na kuunga mkono juhudi za ulimwengu, na kujiingiza katika sekta ya uvuvi kwa kushirikiana na wadau na asasi za kiraia.

Na mwisho, hatua hizi lazima zijengwe kwa kuangalia, na kuboresha juhudi za wizara ya mambo ya nje kupitia idara ya NOAA ambazo zipo katika kushughulikia masuala ya usafirishaji watu katika sekta ya uzalishaji wa chakula cha baharini.

Kukabiliana na usafirishwaji watu katika sekta hii ni jambo muhimu katika haki za binadamu, na masuala ya uhalifu pamoja na vipaumbele vya sera ya mambo ya nje. Ripoti mpya ni hatua muhimu katika kukuza na kuratibu juhudi za Marekani katika kukabiliana na vitendo haramu vya usafirishaji watu katika sekta ya uzalishaji wa chakula cha baharini.

XS
SM
MD
LG