Kama Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo alivyoelezea wazi kwa mara nyingine, ni hadithi ya kuamini tofauti iliyopo kati ya vikosi vya “kijeshi na kisiasa “ vya kundi la kigaidi la Hezbollah.
Hii ni taasisi ya umoja. Hii ni taasisi ya kigaidi, alisema. Linasaidiwa na Jamhuri ya kiislam ya Iran. Na kwa ujumla wake lazima litajwe kuwa ni taasisi ya kigaidi, na ni vyema wahakikishe kwamba wale wote waliohusika na mahusiano kwa Hezbollah wanapaswa kuwekewa vikwazo.
Katika miaka kadhaa iliyopita, mataifa mengi katika jumuiya ya kimataifa ikiwa ni pamoja na Uingereza, Ujerumani, Lithuania, Kosovo, Argentina, Colombia na Paraguay, wanaitambua Hezbollah nzima, sio tu kitengo chake cha kijeshi, kama taasisi ya kigaidi.
Hivi sasa nchi nyingine ya ulaya, Serbia zinakusudia kujiunga na orodha inayoongezeka. Kama sehemu ya makubaliano ya kihistoria kati ya Serbia na Kosovo, ya kurejesha uhusiano wa kiuchumi, Serbia ilitangaza kwamba kwa upana wake itaitaja Hezbollah kwenye orodha yake kama chombo cha kigaidi.
Kosovo ilifanya hivyo hivyo mwezi Juni. Kwa bahati mbaya nchi nyingine vile vile na umoja wa ulaya, zimeshindwa kufanya hivyo, ikikitaja tu kitengo cha kijeshi cha Hezbollah.
Marekani ilikaribisha nia ya dhati ya Serbia. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Pompeo aliita hiyo, ni hatua nyingine muhimu inayozuia uwezo wa kundi la kigaidi linaloungwa mkono na Iran, kuwa na uwezo wa kuendesha harakati zake huko ulaya.
Kizuizi kama hicho katika kile wizara ya mambo ya nje Marekani inakiita “wakala mkuu wa Kigaidi wa Iran” anahitajika kutoa mwangaza kwa mfano, kwa shambulio la kigaidi la mwaka 2012 lililofanywa na Hezbollah huko Bulgaria ambapo watu sita waliuawa, na njama kama ambayo ilifeli huko Cyprus mwaka huo huo. Kwa kuongezea, kama ripoti ya karibuni ya ugaidi ya wizara ya mambo ya nke ilivyosema, kama ilivyokuwa katika miaka iliyopita, serikali ya Iran iliendelea kuunga mkono njama za kigaidi kushambulia wapinzani wa Iran katika nchi kadhaa za bara la ulaya. Katika miaka ya karibuni, Uholanzi, Ubelgiji na Albania wote wamewakamata au kuwafukuza maafisa wa serikali ya Iran wanaohusishwa na njama mbali mbali za kigaidi katika maeneo yao.
Akipongeza uamuzi wa Serbia, waziri wa mambo ya nje Marekani, Pompeo, alisema hakuna shaka kwamba watawala kuvurugika kwa operesheni za Hezbollah za ulaya.
Marekani inaendelea kutoa wito kwa jumuiya ya ulaya na mataifa ya ulaya kultaja au kuipiga marufuku Hezbollah kwa ukamilifu, alisema waziri Pompeo, na kutambua ukweli kwamba ni taasisi ya kigaidi na tawi ambalo halitofautishwi na vitengo vya “jeshi” na a “kisiasa”. Tunazisihi nchi zote za ulaya na kwingineko kuchukua hatua zozote zinazowezekana kuzuia wanachama wa Hezbollah, waajiri na wafadhili kufanya kazi kwenye maeneo yao.