Accessibility links

Breaking News

Siku Ya Polio Duniani


Polio ni ugonjwa hatari wa kupooza na unaoweza kuua unaosababishwa na virusi vya Polio.

Virusi vya polio hushambulia mfumo wa neva na unaweza kusababisha mtu kupooza kabisa katika muda wa saa chache.

Polio unaweza kuathiri mtu yeyote bila kuzingati aumri, lakini Watoto walio na umri wa chini ya miaka 5 ndio walio katika hatari kubwa.

Polio unaweza kuzuiwa kwa kutumia chanjo lakini hauna tiba kabisa mtu anapoambukizwa.

Mnamo mwaka 1988, shirika la afya duniani liliapa kuangamiza polio, ugonjwa ambao umesababisha zaidi ya Watoto 350,000 kupooza katika nchi 125.

Mchango wa shirika la kimataifa la maendeleo la Marekani USAID, ulisaidia kupambana na maambukizi ya virusi vya Polio katika bara la Amerika mwaka 1994, Pacific magharibi mwaka 2000, Ulaya mwaka 2002, Kusini mashariki mwa Asia mwaka 2014 na hivi karibuni,mwaka huu, Barani Afrika.

Katikati ya mwezi Agosti, Afrika ilithibitishwa kutokomeza polio baada ya miaka 4 ya kutotokea kisa chochote kipya cha maambukizi.

Nigeria ilikuwa nchi ya mwisho kuripoti kisa cha maambukizi ya Polio na hivyo kujiunga na nchi 46 katika kanda hiyo kufurahia mafanikio hayo ya kihistoria ya afya ya umma.

Hii leo, visa vya maambukizi ya polio vimepungua kwa asilimia 99.9. Afghanistan na Pakistan pekee ndio nchi zinazoendelea kuripoti maambukizi ya polio.

Katika nchi nyingi, juhudi za kutokomeza kabisa Polio hazijakuwa rahisi.

Migogoro ya kila mara, habari potofu, watu kukoseshwa makwazi, jamii zinazoishi katika maeneo anbayo si rahisi kufikiwa, miongoni mwa changamoto nyingine vimechangia katika kudhoofisha mafanikio dhidi ya polio.

Hata hivyo, iwapo virusi hivyo vitazuiwa kusambaa, lazima juhudi endelevu ziendelee kuchukuliwa.

kupitia tu hali ya kujitolea kabisa, mbinu za ubunifu katika kutatua changamoto na kufanya kazi kwa bidii katika jamii kwa ushirikiano na mashirika ya kimataifa ndiyo njia pekee za kuangamiza kabisa virusi vya Polio duniani.

Kwa ushirikiano maafisa wa afya ambao ni wengi sana kote duniani, viongozi wa kijamii, na wafanyakazi wa kujitolea ambao humfikia kila mtoto, mpango wa USAID wa kutokomeza polio kote duniani, umesaidia kuhakikisha kwamba zaidi ya Watoto milioni 400 wamepata chanjo dhidi ya Polio kila mwaka.

Hii leo, karibu watu milioni 19 waliokuwa katika hatari kubwa ya kupooza kutokana na polio,wana uwezo wa kutembea na zaidi ya watu milioni 1.5 wapo hai baada ya kunusirika kifo kutokana na polio.

Mwaka huu 2020, ni mwaka wa kipekee katika kusherehekea siku ya polio duniani baada ya kupatikana mafanikio makubwa sana kutokana na Afrika kutokomeza kabisa ugonjwa huo licha ya janga la virusi vya Corona kuendelea kutatiza mfumo wa afya kote duniani, ikiwemo mipango ya kutoa chanjo.

USAID na washirika wake, wanapanga kutumia yale wamejifunza katika kupambana na Polio katika kupambana na janga la sasa la Corona na milipuko mingine ya magonjwa hatari inayoweza kutokea katika siku zijazo.

XS
SM
MD
LG