Accessibility links

Breaking News

Slovania yauweka muundo mzima wa Hezbollah katika orodha ya kigaidi


Ifwatayo ni tahariri inayoelezea sera na maoni ya serekali ya Marekani.

Slovania imelitaja kundi la Hezbollah kwa muundo wake mzima kama taasisi ya kigaidi, ikitupilia mbali maelezo kwamba kuna tofauti katiy a Hezbollah, tawi la kisiasa na tawi la kijeshi.

Kama alivyoeleza Waziri wa Mambo ya Nje wa Slovenia Hezbollah ni kundi la kihalifu na kigaidi ambalo linatishia amani na usalama wa dunia.

Marekani inaipongeza Slovania kwa kuchukua hatua hii ili kusaidia kuizuia Hezbollah kuendesha shughuli zake barani ulaya.

Slovania imefuata nyayo za serekali nyingine za ulaya ikiwemo Uingereza, Lithuania, Latvia, Kosovo na Estonia ambazo zote zimechukua hatua muhimu kulitaja, kulipiga marufuku na kulizuia Hezbollah katika miaka kadhaa iliopita.

Tangu lililopoundwa na utawala wa Iran mwaka wa 1982, kundi la Hezbollah liliendeleza mtandao mbaya unaojumuisha mbinu za kisiasa, kijeshi, kigaidi na kihalifu. Hezbollah iliunda jeshi kubwa la kigaidi lenye ma elfu ya wapiganaji, likiripotiwa kumiliki roketi na makombora laki 1 na elfu 30.

Zaidi ya hayo, Hezbollah ilianzisha mtandao wa kimataifa wa kigaidi na kihalifu kutoka Amerika kusini hadi ulaya, mashariki ya kati na Asia.

Hezbollah ina historia ndefu ya ugaidi na mashambulizi ya kigaidi dhidi ya maslahi ya ulaya. Tangu miaka ya 1980, imeendesha msururu wa mashambulizi ya kigaidi dhidi ya malengo ya ulaya nchini Lebanon, na ulaya, ikiwemo Ufaransa, Spain, ujerumani, Bulgaria, na Cyprus.

Hezbollah iliunda miundo mbinu mipana kwa ajili ya shughuli za kigaidi kwenye ardhi ya ulaya, na kuendesha mitandao ya uhalifu wa kifedha kote barani ulaya, ikiwemo biashara ya dawa za kulevya, utakatishaji pesa, na uhalifu wa mitandaoni.

Hezbollah ilituma wanajeshi wake kupigana katika vita vya Bosnia mwanzoni mwa miaka ya 1990.

Utawala wa rais Donald Trump ulianzisha harakati za kidiplomasia kuishawishi jumuia ya kimataifa kufuatilia kwa makini shughuli mbaya za Hezbollah na kulizuia kundi hilo linaloungwa mkono na Iran, kuendesha operesheni zake ndani ya nchi kwenye maeneo hayo.

“Tumeweka msisitizo maalum kwa bara la ulaya”, amesema waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo katika taarifa. Na kampeni ya kidiplomasia inayoongozwa na wizara ya mambo ya nje, imezaa matunda, kukiwa nchi 6 za ulaya ambazo ziliiwekea vikwazo kundi la Hezbollah mwaka uliopita, huku serekali nyingine za ulaya zikifikiria uwezekano wa kuchukua hatua mpya.

Marekani inapongeza hatua hizi zilizochukuliwa na Slovenia, na nchi nyingine za ulaya kama hatua nzuri ya kutokomeza kuwepo kundi la Hezbollah ndani ya bara la ulaya.

XS
SM
MD
LG