Accessibility links

Breaking News

Syria Inataka Wakimbizi Warejee, Russia Inaunga mkono


Ifuatayo ni tahariri inayoelezea sera na maoni ya serikali ya Marekani. 

Kwa takribani miaka kumi, Syria imekuwa ikiwanyanyasa watu wake kwa njia mbaya sana kadri iwezekanavyo. Utawala ukiongozwa na Bashar al Asaad, unawashambulia waandamanaji wa amani kwa vifaru na bunduki. Ilidondosha mabomu ya petrol pamoja na vilipuzi vingi kwa watu wake na kuuwa watu katika eneo zima la ujirani na vijiji kwa kutumia gesi ya sumu. Raia wa Syria walikatwa viungo, kuteswa na kufa kwa njaa, kemikali na kupigwa risasi. Huko Syria, raia hawakuuwawa kwa vita pekee, lakini pia walikuwa walengwa.

Matokeo yake, kati ya idadi ya watu milioni 23 kabla ya vita, takribani watu laki tano wameuawa, watu milioni 6.5 wamekoseshwa makazi wakati wengine milioni 5.6 ni wakimbizi katika nchi jirani. Lakini hivi sasa, Assad ambaye ni mbunifu wa ukatili huu anatoa wito kwa wakimbizi hao kurudi Syria. Madai yake haya yakiungwa mkono, na mfuasi wa karibu na pia mwezeshaji wake Rais wa Russia, Vladimir Putin.

Katika mkutano wa karibuni kuhusu wakimbizi uliofanyika mjini Damascus na kuandaliwa pamoja na Syria na Russia, Assad na Putin walisisitiza kwamba vita vya wenyewe kwa wenyewe vimekwisha na kwamba maeneo mengi ya nchi hiyo yaliyoharibika, hivi sasa yako na Amani. Wakati huo huo, Russia ilisisitiza ujenzi mpya wa nchi iliyoharibiwana vita lazima uambatane na kurudi kwa wakimbizi wa Syria, ikidai kwamba wakimbizi wataweza tu kurudi nyumbani, kama mataifa ya Magharibi yapo tayari kulipa fedha ili kuijenga tena Syria. Hili ni jaribio la wazi lililofanywa na Russia kuingiza pesa kwa kuyasaidia makampuni yake kunasa mikataba yenye faida kubwa katika ujenzi mpya.

Wakimbizi hawaamini ahadi za Assad. Mataifa ya magharibi pia hayakubaliani na hilo na yanasisitiza kwamba fedha za ujenzi mpya zitapatikana tu wakati wafungwa wote wa kisiasa wanapoachiliwa, kuwepo na hakikisho la usalama kwa wa-Syria wote na mchakato wa kisiasa nchini Syria unachukuliwa kuwa halali.

Utawala wa Assad, kwa kuungwa mkono na Russia unataka kutumia mamilioni ya wakimbizi walio katika mazingira magumu kama mikono ya kisiasa katika jaribio la madai ya uongo kwamba mzozo wa Syria umekwisha, alisema naibu msemaji wa wizara ya mambo ya nje Marekani, Cale Brown katika taarifa ya maandishi.

Utawala wa Assad unahusika kwa vifo zaidi ya laki tano vya raia wake wenyewe, kwa kupiga mabomu hospitali kadhaa na kuwanyima msaada wa kibinadamu mamilioni ya raia wa Syria. Hizi sio hatua za serikali ambayo inaweza kuaminiwa kuamua ni lini wakimbizi wanaweza kurejea salama nchini mwao, wala Assad hapaswi kuwepo madarakani kutoa mwongozo wa fedha za kimataifa juu ya ujenzi mpya , alisema.

Marekani inaendeleza nia yake ya dhati ya kujitolea kwa watu wa Syria, na kwa azimio namba 2254 la Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo ndio njia pekee ya suluhisho la kisiasa kwa mzozo wa Syria.

XS
SM
MD
LG