Accessibility links

Breaking News

Ulimwenge waadhimisha siku ya kumalizika Vita vya Pili vya Dunia


Ifuatayo ni tahariri inayoelezea sera na msimamo wa serikali ya Marekani

Septemba 2, ulimwengu unaadhimisha siku ya kumalizika kwa vita vya pili vya dunia katika kanda ya Pacific, na hivyo kumaliza mgogoro wa dunia. Miaka 75 iliopita, hati rasmi za kujisalimisha bila masharti kwa Japan zilisainiwa na Marekani na Japani, ndani ya meli ya USS Missouri, ilipotia nanga kwenye pwani ya Tokyo Bay.

Baada ya Ujerumani kujisalimisha tarehe 8 May, vita vya pili vya dunia vilimalizika huko ulaya.

Pamoja na hivo, vita vilivyokua vinapamba moto katika kanda ya Pacific, vita hivyo visingemalizika bila Japan kuweka chini silaha.

Tarehe 26 Julai, siku 10 baada ya Marekani kufanya jaribio la bomu ya atomic, viongozi wa mataifa shirika ya marekani walitoa tamko ambalo ni hati inayoelezea masharti ya kujisalimisha kwa ufalme wa Japan.

Endapo Japan ingekata pendekezo hilo, ingepata madhara makubwa kwa haraka na kuangamizwa kabisa. Japan ilikata kupewa shinikizo.

Kwa hivyo ikawa muhimu kuishinda Japan kwenye uwanja wa vita, hakika ilikua kazi kubwa. Kwa kipindi cha miaka 3, Marekani na washirika wake katika kanda ya Pacific walipambana na Japan katika moja ya vita vya majeshi ya majini katika historia.

Mapambano makali katika visiwa vya Pacific, ambayo mara nyingi hayakupelekea wanajeshi wa Japan walioshindwa vile vile na raia kujimalizia maisha kwa wingi, yalifanya uongozi wa kijeshi wa marekani kuamini kwamba uvamizi wa Japan, utasababisha maafa makubwa pande zote mbili.

Kwa hivyo iliamuliwa vita vimalizike haraka.

Baada ya kusambaza nyaraka zinazoonya kuhusu mashambulizi makali ya angani na kutaka raia waondoke kwenye maeneo yao, marekani iliangusha mabomu mawili ya atomic kwenye miji miwil ya Japan, kwa siku 3.

Mwishowe, uongozi wa Japan uliamini kuwa vita haviwezi kushinda, na terehe 14 Agosti, mfalme wa Japan Hirohito akatangaza kwamba Japan itajisalimisha.

“Leo silaha ziko kimya, jenerali Douglas MacArthur aliekubali kujisalimisha kwa Japan kwa niaba ya majeshi ya ushirika, alisema katika sherehe za kumaliza vita akiwa ndani ya meli ya USS Missouri.

“Janga kubwa limemalizika. Ushindi mkubwa umepatikana. Anga kamwe haina mvua ya vifo, bahari imebeba biashara – wanaume kila mahali wanatembea vifua mbele. Dunia nzima imekaa kimya kwa amani. Kazi muhimu imekamilika.

Katika ukanda wa pacific yamekuja mafanikio kwa dunia mpya iliyo huru. Leo, uhuru unashambuliwa, demokrasia inaandamwa. Leo huko Asia pamoja na Ulaya, watu waliofunguliwa wanaonja utamu wa ukombozi, ahueni kutoka katika woga.”

Tarehe 2 Septemba, mwaka wa 1945, hatimae vita vya pili vya dunia vilikua kweli vimemalizika na enzi mpya ikaanza.

“ Hiyo ilikua ni tahariri inayoelezea sera na msimamo wa serekali ya Marekani”

XS
SM
MD
LG