Accessibility links

Breaking News

Ushirikiano Kati Ya Marekani Na Bahrain Waendelea Kuimarika


Marekani na Bahrain wamekuwa na uhusiano wenye nguvu kwa miongo kadhaa. December 1, nchi hizo mbili zilizindua mjadala wa kwanza wa kimkakati, ulianza kwa matamshi yaliyotolewa katika ufunguzi wa kikao hicho kwa njia ya mtandao na waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo na waziri wa mambo ya nje wa Bahrain, Abdullatif bin Rashid Al Zayani.

Waziri Pompeo aliipongeza Bahrain kwa kutia saini mkataba wa kihsitoria Abraham Accords, ambao unarejesha uhusiano wa kawaida na Israel, ikiwa ni moja ya nchi nne kufanya hivyo, kwa kufungua ushirikiano katika maeneo mengi, ikiwemo utalii, elimu, biashara na usalama.

“Hii ni dalili ya matumaini kwa eneo hilo kwa vile linaondoka katika kipindi kilichopita, mawazo yaliyopitwa na wakati ambako hakuna anayetaka kurejea. Nina imani mataifa mengi zaidi yatafuata mfano wa uongozi wa Bahrain, kuonyesha ukubwa wa kijiografia wa nchi si kigezo cha kuonyesha ushawishi katika uwanja wa dunia,” amesema waziri Pompeo.

Kwa kuongezea, waziri Pompeo amezungumzia jukumu la Bahrain kama mshirika wa ulinzi kwa Marekani. Ameelezea kuwa msaada wa Bahrain katika kuishinda ISIS kwa kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya ukhalifa wa uongo, na ameelezea jukumu la Bahrain kuwa mwenyeji wa kikosi cha kamandi ya jeshi la majini la Marekani na makao makuu ya kikosi cha Fifth Fleet cha Marekani.

Hiyo inaturuhusu kushirikiana katika mambo mengi, kuanzia mapambano ya ugaidi, mpaka kulinda njia salama za usafirishaji wa bidhaa katika Ghuba, mbali na mashambulizi ya baharini kutoka Iran.”

Waziri Pompeo alielezea kwamba utawala wa Iran ‘ni tishio la kwanza kwa usalama wa Ghuba na kwa watu wanaopenda amani kote katika eneo hilo.”

“Tunataka kuishukuru Bahrain na watu wake kwa msaada wao wa haraka katika kampeni yetu, ambapo kwa mafanikio tumeitenga Tehran na kuzuia mabilioni ya dola kwa Iran ili kuzitumia kwa ushawishi na vitisho,” waziri Pompeo amesema.

Kile ambacho Bahrain na Marekani wanashirikiana amesema waziri Pompeo ni ‘sera muhimu ya mambo ya nje. Sisi ni wakweli, tunaiona dunia kama ilivyo.’

“Tunatambua hali ya ghasia katika utawala wa kimapinduzi wa Iran, na tunaelewa kwamba linapokuja suala la kukabiliana na Tehran na masuala mengine muhimu, Israel ni mshirika muhimu, na siyo tatizo.” Amesema waziri Pompeo.

Katika kipindi cha wiki kadhaa zijazo, makundi matano ya kikazi kutoka wizara ya mambo ya nje na mashirika mengine ya Marekani yatakutana na wenzao wa Bahrain kujadili maeneo kama vile mafunzo ya kijeshi, uwezeshaji wanawake, haki za binadamu, na hatari zinazoletwa na hali ya baadaye ya mitandao ya 5G ya chama cha kikomunisti cha China.

Waziri Pompeo amesema ana imani kwamba vikao hivi vitaweka msingi kwa ushirika wenye nguvu zaidi kati ya Marekani na Bahrain.

XS
SM
MD
LG