Accessibility links

Breaking News

Utawala wa Maduro Wadaiwa kutenda Uhalifu Mkubwa Dhidi ya Haki za Binadamu


Ifuatayo ni tahariri inayoelezea sera na maoni ya serikali ya Marekani.

Tume ya kimataifa ya Kujitegemea ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kwa Venezuela, imetoa ripoti mwezi Septemba, ikihitimisha kwamba kuna ushahidi wa kuaminika kwamba uhalifu dhidi ya ubinadamu ikijumuishwa makosa dhidi ya ubinadamu ya mauaji, kuwafunga gerezani, kutesa, kulazimisha watu kukimbia makazi yao, ubakaji na makosa mengine ya udhalilishaji wa kijinsia, yalifanyika nchini Venezuela.

Cha kusikitisha zaidi, ripoti ya Umoja wa Mataifa, inaeleza kwamba “ina ushahidi wa kutosha kuamini kwamba rais na mawaziri wanaohusika na masuala ya ndani ya watu, sheria, na amani, pamoja na ulinzi, waliamuru ama kushiriki kufanyika kwa makosa yaliyoandikwa katika ripoti.” Kwa maneno mengine, ukiukwaji huo wa haki za binadamu umeanzia katika ngazi za juu.

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, liliunda tume ya kutafuta taarifa mwezi Septemba mwaka 2019. Mamlaka yake yalikuwa kuchunguza mauaji holela, kulazimishwa watu kukimbia makazi, watu kushikiliwa bila makosa, na mateso, ikijumuisha unyama mwingine, kutokuwepo kwa ubinadamu, ama unyanyasaji toka mwaka 2014, ikifanya jukumu la kuweka mazingira ya kuwafikisha wote waliohusika mbele ya sheria.

Taarifa hiyo katika ripoti ya Umoja wa Mataifa inaonyesha haja ya kuwepo kwa mabadiliko ya kidemokrasia ambayo yako huru na wazi nchini Venezuela. Ni njia pekee kumaliza manyanyaso ya Wavenezuela walio katika mikono ya serekali isiyo halali ya Nicolas Maduro, na kuleka haki kwa waathirika wa unyama na manyanyaso ya utawala wake. “Marekani ipo pamoja na watu wa Venezuela, ambao wanastahili kuishi bila ghasia kutoka kwa wale ambao wanapaswa kuwalinda, na kuwahudumia.” Amesema kaimu mkuu wa USAID, John Barsa katika taarifa yake.

Rais wa mpito, Juan Guaido, na serekali yake, wabunge wa bunge lililochaguliwa kidemokrasia, asasi za kiraia za Venezuela, watetezi wa haki za binadamu, na vyombo vya habari vilivyo huru vinajukumu kubwa katika kuendeleza demokrasia ya Venezuela. “Ni mashujaa halisi.” Amesema kaimu mkuu Barsa, “Na nina uhakika kwamba watafanikiwa.”

Jumuiya ya kimataifa lazima iungane kwa ajili uchaguzi ulio huru na haki wa rais na wabunge na kurejesha utawala wa kidemokrasia nchini Venezuela. Marekani inatazamia siku ambayo itasherehekea kurejea kwa uhuru, na kuheshimiwa kwa haki za binadamu nchini Venezuela.

XS
SM
MD
LG