Mwezi Agosti, serekali ya Marekani imedhamiria kulinda taasisi za kitaaluma za Marekani kutoingiliwa na ushawishi wa chama cha Kikomunisti cha China, na kulinda uhuru wa taaluma kwa kuitambua taasisi ya kituo cha taasisi ya itikadi mjini Washington DC, ama CIUS, kama tume ya kigeni ya Jamuhuri ya watu wa China.
Hatua hiyo imeweka waazi kwamba CIUS, kama waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo alivyosema, sehemu ya “propaganda ya Beijing, na kituo cha kuratibu kampeni za ushawishi kwenye vyuo vya elimu ya juu vya Marekani, na madarasa ya kuanzia ya chekechea mpaka darasa la 12.”
Mwezi Septemba, serekali ya Marekani ilitangaza hatua nyingine kuilinda Marekani na udhalimu wa serekali ya China.
Katika hotuba iliyoelezea vitisho vinavyowekwa na chama cha kikomunisti cha China, ikijumuisha wizi wa haki za kitaaluma, ubunifu wa viwandani, na kuiba taarifa binafsi za raia wa Marekani, kaimu waziri wa usalama wa ndani Chad Wolf, alisema Marekani pia itakabiliana na jaribio la China kutumia taasisi za elimu za Marekani kwa kusitisha vibali vya kuingia Marekani kwa wanafunzi wa Kichina ambao wamekuwa wakisoma Marekani, na kuwa na uwezekano wa kuleta hatari kwa usalama wa taifa.
“Tunazuia viza kwa baadhi ya wanafunzi wa shahada za juu, na watafiti wenye uhusiano na idara za kimkakati za jeshi ili kuwazuia kuiba, na uwezekano wa kutumia vibaya tafiti.”
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani amesema hatua hiyo kwa viza ilifuatia na kupewa baraka na rais Donald Trump, hapo Mei 29 kwa kuithinisha hatua hizo kwa sababu serekali ya China inatumia shughuli kama hizo za baadhi ya wanafunzi wa China kuweka hatari katika maslahi ya Marekani.
“Mpaka ilipofika Septemba 8, 2020, msemaji huyo amesema katika taarifa yake kwamba “wizara hiyo imefuta viza zaidi ya 1,000 za raia wa Jamuhuri ya watu wa China ambao wameguswa na tangazo la rais la 10043, na kuzifanya kutokuwa vibali vya kuwepo kwa Marekani kama wanafunzi.
Kuna raia wa China 360,000 wanasoma Marekani. Wizara ya mambo ya nje imesema viza 1,000 zilizofutwa kwa wanafunzi wa shahada za juu wenye wenye hatari, na watafiti” ni sehemu ndago ya asilimia ya wanafunzi hao. “Tunaendelea kukaribisha wanafunzi wenye nia njema, na wanazuoni kutoka China, ambao hawana uhusiano na chama cha kikomunisti na malengo yake ya kuongeza ushawishi wa kijeshi.
Kaimu waziri wa usalama wa ndani Wolf, alitangaza kwamba chama cha kikomunisti cha China kimeeleza kila Nyanja ya nguvu yake katika kudhoofisha demokrasia, na nia yake ya kuleta mfumo mpya duniani kwa namna yake ya picha ya kiimla.
Lakini, ameeleza kwamba, Marekani inaendelea kuonyesha kwamba “japokuwa hatua hizo za China zinaweza kuwa na uhatari, lakini hazitofanikiwa.”