Katika maadhimisho ya 41 ya kukamatwa kwa u balozi wa Marekani mjini Tehran, Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo ameelezea kwamba utawala wa Iran kuendelea kushikilia mateka na kuendeleza ajenda zake mbaya.
Ameitaka Iran kuwaachia raia wa Marekani wanaozuiliwa kimakosa, Morad Tahbaz na Siamak na Baquer Namazi, na pia kuelezea hatima ya afisa wa FBI Robert Levinson ambaye alitekwa nyara miaka 13 iliyopita.
Lakini kama Waziri Pompeo alivyotangaza, “Hawa raia wasio na hatia siyo tu waathirika wa utawala dhalimu wa Iran – na waathirika wa muda mrefu ni watu wa Iran, na wao wanastahili hali nzuri zaidi.”
Ripoti ya karibuni ya Javaid Rehman, mwandishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Iran anaunga mkono tathmini ya waziri Pompeo.
Katika maoni yake kwenye mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa kamati ya tatu kwenye ripoti yake, Bwana Rehman amesema kuwa hali ya haki zaz binadamu nchini Irn inaweza kuelezewa ni ‘mfumo wa ukiukaji wa haki za binadamu na kutokhaofia kushtakiwa.”
Akielezea majibu ya nguvu ya utawala kwa maandamano ya mwaka jana dhidi ya serikali ambapo mamia ya watu waliuawa, Bwana Rehman amesema Iran “lazima ifanya uchunguzi huru, usioelemea upande wowote na wa wazi kuhusiana na msako uliotumia nguvu kubwa dhidi ya maandamano ya November mwaka 2019 na Januari 2020, na kuwafikisha mbele ya sheria wakiukaji wa haki za binadamu.”
Lakini ivtendo vya utawala vinaonyesha kwamba uwazina sheria ni vitu ambavyo wala hawavitilii maanani.
“Kitumia mateso na adhabu kali sana dhidi ya wale ambao waliandamana; kuwanyanyasa waathirika wanaodai haki, na ukosefu wa uwajibikaji kwa wale waliohusika.”
Mwandishi Maalium Rehman pia alielezea adhabu za vifo ambazo zimetolewa kwa waandamanaji baada ya kulazimishwa kukirimakosa na vifungo vya muda mrefu kwa wafungwa wa siasa ikiwa ni pamoja na mawakili, waandishi wa habari, wanamazingira na watetezi wa haki za binadamu.
“Mwenendo wa Dhahiri unajibainisha ikiwa ni jaribio la kunyamazisha upinzani wa umma juu ya hali ya kijamii, kiuchumi na kisiasa nchini Iran.”
Kama Waziri Pompeo alivyowaeleza viongozi wa Iran “Mafanikio ya kweli yatakuja pale tu Iran mtakapoacha kuwatisha raia. Wenu na kuwafunga. Watendee watu wenu kwa kuwapa heshima, jambo ambalo kila binadamu anastahili.”