Accessibility links

Breaking News

Zaidi ya kile kinachojulikana kuhusu Shirika la Afya Duniani


Ifuatayo ni tahariri inayoelezea sera na maoni ya serikali ya Marekani.

Marekani kwa muda mrefu imekuwa ni mkarimu mkubwa kwa misaada ya afya na kibinadamu kwa watu kote duniani. Msaada huu unatolewa kwa msaada wa walipa kodi wa Marekani kwa matarajio kuwa utakuwa na matarajio ambayo yakidhi malengo na kuwafikia wale wenye shida.

“Bahati mbaya, Shirika la Afya Duniani, au WHO, imeshindwa vibaya kwa hatua hizo, siyo tu katika majibu yake kwa Covid 19, lakini kwa mizozo mingine ya afya katika miongo ya karibuni,” amesema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Morgan Ortagus katika taarifa yake. “Kwa kuongezea, WHO, imekanusha kupitisha mageuzi haraka, kuanzia kuonyesha uhuru wake kwa chama cha kikomunisti cha China.”

Matokeo yake, Marekani kujiondoa rasmi kutoka Who ifikapo July 6, mwaka 2021.

Nia ya dhati ya Marekani kwa msaada wa afya nje ya nchi bado ni wenye nguvu. Wakati utawala ukielekea kujiondoa rasmi, wanaangalia njia za kuongeza utalaamu muhimu wa wizara na idara za serikali ya Marekani na sekta binafsi za Marekani kutoa msaada muhimu haraka kwa nchi nyingine ili kuzuia, kugundua, na kujibu milipuko ya magonjwa ya kuambukiza kwenye chanzo chake na dharura za kibinadamu.

Tangu mwaka 2001, serikali ya Mrekani imechangia zaidi ya dola bilioni 42 ili kusaidia kuzuia, kugundula na kutibu HIV na Ukimwi, malaria, kifua kikuu, ebola, na magonjwa mengine hatari sana. “Tunatoa wastani wad ola bilioni 10 kwa mwaka kwa afya ya ulimwengu, na mwaka huu, itaongeza marambiliya kiwango hicho wakati tukongeza mapambano ya Covid 19 kote duniani,” amesema Afisa msaidizi wa masuala ya afya ya uliwmengu katika USAID, Dr. Alma Golden.

Marekani ina azma ya kuhakikisha kwamba kujiondoa kwake kutoka WHO hakutaathiri kiwango cha jumla cha msaada kwa wale walio katika mazingira hatarishi.”Marekani inaiongoza duniani katika misaada ya afya na ya kibinadamu kupitia juhudi zote za Marekani,” ameongeza Dr. golden, “na tuna nia ya dhati ya kuhakikisha kwamba ukarimu wetu moja kwa moja unawafikia watu kote duniani.”

XS
SM
MD
LG